HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » TASWIRA ZA MECHI YA KILIMANJARO STARS VS SOMALI DEC 1, 2012 HUKO UGANDA.

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakisalimiana na wachezaji wa Somalia kabla ya kuanza mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda
.
Mrisho Ngassa akipongezwa na Athuman Idd baada ya kufunga goli la kwanza, ambapo Tanzania ilishinda 7 – 0 Mrisho Ngasa akifunga magoli matano na John Bocco mawili.
Mrisho Ngasa wa Kilimanjaro Stars mwenye mpira akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Somalia wakati wa mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda.
Beki wa Kilimanjaro Stars, Erasto Nyoni akiambaa na mpira wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge dhidi ya timu ya Somalia uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda.
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars Mrisho Ngassa akiambaa na mpira uliozaa goli la kwanza sekunde ya 48
Mrisho Ngassa akishangilia moja ya goli kati ya matano aliyofunga wakati wa mchezo na Somalia uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, John Bocco (kulia) akimtoka beki wa timu ya Somalia, Abdallah Mohamed
Boko akishangilia moja ya goli wakati wa mchezo na Somalia
Mashabiki wa Tanzania
 Ripoti ni ya Shaffih Dauda.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: