BERENIKI KIMIRO; Mshindi wa Maisha Plus 2012

 
Mshindi wa Maisha Plus 2012 kutoka Dar es salaam ni BERENIKI KIMIRO, amejishidia Tshs. Millioni 20. Mshindi wa Maisha Plus 2012, BERENIKI KIMIRO alianza kwa Kumshukuru Mungu kwa ushindi, asema ye si kitu kwa wenzake, hilo ni zali tu.. Amemshukuru baba yake mzazi kwa kumshauri kusali. Aliwashukuru pia wapenzi watazamaji kwa kumpiga kura, ameahidi kuendeleza kile alichokianzishaa kijijini na kuitendea haki nchi yake Alimshukuru babu, Brother Masoud na Crew nzima ya Maisha Plus.. Alimshukuru pia mwanae Kelvin (6yrs) kwa kuvumilia kipindi chote bila kuongea na mama. Alisema Mungu amejibu maombi yake kwani ukipiga goti, maombi yako yatajibiwa.. Tutawapa taarifa kupitia ukurasa huu kuhusu hali ya Bereniki ambaye  alionekana amezimia.
Venance Mushi
Mshindi wa Pili ni Venance Mushi kutoka Dodoma amejishindia Tshs. Million 6.
 Justin Bayo
Mshindi wa Tatu ni Justine Bayo, kutoka Morogoro amejishindia Tshs. Million 4.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu aliitwa kusema machache pamoja na kutangaza Mshindi wa Maisha Plus 2012.. Masoud Kipanya, alimkaribisha, akishukuru kwa zawadi aliyoitoa ya ya Tshs. Millioni 10 ambayo itagawanyika Millioni 6 kwa Mshindi wa Pili na Million 4 kwa mshindi wa tatu.
 Mhe. Nyalandu aliongezea zawadi ya Tshs. Million 7.5 ili igawanywe Tshs. Laki tano kwa kila mshiriki ambaye hakuingia top 3, aliwakaribisha pia washiriki wote kwa chakula cha Mchana siku ya kesho katika hoteli ya Serena.

No comments

Powered by Blogger.