HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » TUMETOKA MBALI MPAKA KUPATA UHURU 1961

Happy Uhuru Day!

Tunakukumbusha tulikotoka...

Pichani ni Tabora Railway Station, mwaka 1966...
Pichani ni Tabora Railway Station, mwaka 1966.

Happy Uhuru Day!

Hawa pichani si CHADEMA (sababu ya 'V' sign), ni wanafunzi wa Kisutu Girls mwaka 1975...

Tumetoka mbali :)
Hawa pichani si CHADEMA (sababu ya 'V' sign), ni wanafunzi wa Kisutu Girls mwaka 1975.
 Happy Uhuru Day!

Tumetoka mbali... Pichani ni basi la 'Tanganyika Bus' (enzi za miaka ya 1960s) lililokuwa likifanya safari kati ya Mwanza na Arusha

Kwa wale wenyeji wa Mkoa wa Kagera, hapa ni Bukoba mjini mwaka 1972

Enzi hizo...

Stendi ya mabasi Mwanza to Musoma early 1960s...

Tumetoka mbali :)
Stendi ya mabasi Mwanza to Musoma early 1960s.
Happy Uhuru Day!

Picha hii ilipigwa siku chache kabla ya Uhuru wa Tanganyika
Picha hii ilipigwa siku chache kabla ya Uhuru wa Tanganyika
 Happy Uhuru Day!

Tunakukumbusha tulikotoka...

Pichani ni Sokoine University of Agriculture(SUA) mwaka 1971
Pichani ni Sokoine University of Agriculture(SUA) mwaka 1971
Happy Uhuru Day!

Tunakukumbusha tulikotoka... Pichani ni uwanja wa ndege wa Biharamulo (Mkoani Kagera, enzi hizo Ziwa Magharibi) mwaka 1958

UHURU WETU, SHEREHE ZENYE HESHIMA NA KUMBUKUMBU YA MAPAMBANO MAZITO YA WAZALENDO.

NAMNA ILIVYOKUWA MWAKA 1961.

Pichani ni aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam na Kiongozi wa Shughuli za Sherehe za Uhuru wa Tanganyika (sasa Tanzania Bara) Sheikh Amri Abeid Kaluta (Aliyesimama akihutubia) akiongoza.

Kulia wa kwanza aliyekaa ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha TANU Bwana Oscar Salathiel Kambona akifuatiwa na Rais wa Chama cha TANU na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Tanganyika (na sio Waziri Mkuu) Ndugu Julius Kambarage Nyerere.

Wa tatu Kulia Mwenye Suti ni Gavana wa Mwisho wa Tanganyika Sir Richard Turnbull, Mume wa Malkia wa Uingereza na Bwana Jumbe wa Edinburgh (Duke of Edinburgh) Prince Philip ndiye anayefuatia (Wa nne Kutoka kulia waliokaaa, Mwenye Mavazi ya Kijeshi), na wa tano Kulia ni Mke wa Gavana Turnbull.

Sherehe hizo zilifanyika katika Uwanja wa Uhuru (Zamani Uwanja wa Taifa) Jijini Dar es salaam Tarehe 9 Disemba, 1961 ambapo Prince Philip ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo na ndiye aliyekabidhi Uhuru kwa niaba ya Mkewe Malkia wa Uingereza.

HAMASA YA WANANCHI.

Kwa watanganyika wengi ambao walikuwepo wakati huo Uhuru ulikuwa na maana kubwa na nzito sana kwao, ukitambulika kama Fursa ya Ukamilifu wa Utu wao na pia Ujenzi na Msingi wa kujenga Taifa Taifa imara lenye kuongozwa na Watu waadilifu kwa Misingi ya Haki, Utu na Usawa.

Fikra za mambo yote hayo ziliongeza na kuchochea hamasa nyoyoni mwa Wananchi hawa wa Tanganyika na kuiamsha kwa dhati ari ya kujenga taifa jipya na kulitumikia kwa Uzalendo, Uadilifu, Uaminifu kwa juhudi na Maarifa makuu.

Uhuru huu ulitazamwa kwa jicho jengine kama fursa ya kuwaletea maendeleo wana Taifa wengi wanyonge ambao kwao Ukoloni ulichochea hali zao za Kitwana na kuwajengea Matabaka ya dhahiri kati ya walionacho na wasionacho, Uhuru uliibua Matumaini ya kuendelea Kiuchumi kama Taifa na kuweka Misingi sawa ya Ulaji keki ya Taifa.

SAFARI YENYE MAFUNZO.

Leo ni Miaka 51 tokea tukio hili adhimu litokee katika ardhi ya Nci adhimu, Asubuhi ya Leo wananchi mbalimbali walirudi tena katika Uwanja huu huu wa Uhuru kuadhimisha na kusherehekea Kumbukumbu njema ya siku hii muhimu kwa Utaifa wetu.

Marejeo hayo si tu yalimaanisha furaha, jadi na usuli wa maadhimisho bali yalikumbusha juu ya safari ndefu na yenye mafunzo iliyoanzwa na Wazee wetu wazalendo Miaka 51 iliyopita.

Maadhimisho hayo huchukulika kama Mafunzo ya kudurusu maisha yetu kama Taifa miaka 51 iliyopita kwa kudonoa yale mambo yetu muhimu na ya kimsingi ambayo aidha tunapaswa kuyaiga kutoka kwa Wazee wetu kwa tija yake kwa Taifa au kuyarekebisha kwa kuwa ni sehemu ya makosa yao kama wananadam.

Ni wakati muafaka kwa kila mmoja wetu kufanya mrajaa huo kwa mustabali mwema wa Taifa hili miaka mingine 51 ijayo.

Ukurasa wa Watanzania Mashuhuri unawatakia Furaha, Umoja, Amani na Mshikamano wa Kumbukumbu hii ya Miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: