Rais
wa Jamhuri ya Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipinga mkono kuwasalimia
wananchi wakati akiingia kwenye uwanja wa Uhuruy, leo wakati wa sherehe
za maadhimidho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania. Picha zaidi za matukio
zitawajia baadaye
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya
Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya
maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila
mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji,
Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika
maadhimisho hayo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika
maadhimisho hayo
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama kikitumbuiza katika maadhimisho hayo
Viongozi
mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph
Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mama Maria Nyerere, Rais wa
Msumbiji Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. Gharib Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa
awamu ya pili
Rais
wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza akipokewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa.
Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mh. Joseph Kabila akipokewa na
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili
kwenye uwanja wa Uhuru asubuhi hii.
Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili
kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.
Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho hayo.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii
na heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya
Tanzania Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu
wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada
ya kuwasili uwanjani hapo, katikati ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Rais
Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya
miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru
jijini Dar es salaam akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na
ndani ya nchi
Rais
Dk. Jakaya Kikwete kulia akipokea Gwaride la Heshima lililpokuwa
likipita mbele yake wanaofuatia katika picha ni Rais wa Zanzibar Dk.
Mohamed Shein, Rais wa Namibia Mh. Ifikepunye Pohamba na Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete wakiwa katika maadhimisho hayo
Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Hapa wakionyesha ukakamavu wao huku wakiwa wameshika silaha.
Kikosi
cha wanaanga Jeshi la wananchi JWTZ kikitoa heshima kwa gwaride kali
mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania
Dk. Jakaya Kikwete
Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ kipita kwa gwaride la heshima mbele ya Rais Dk. Jakaya Kikwete.
CHANZO: FULLSHANGWEBLOG.COM





No comments:
Post a Comment