Waziri Mkuu Mstaafu na Mwanasiasa Mkongwe nchini, John Malecela
ASEMA LICHA YA KUSTAHILI KUWANUFAISHA WATANZANIA WOTE,UKIWA KARIBU NA WARIDI UNATAKIWA KUNUKIA
WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwanasiasa Mkongwe
nchini, John Malecela, ametoa wosia kuhusu mgogoro wa gesi akiiomba
Serikali kufanya kila iwezalo ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mtwara
wananufaika kwanza na rasilimali hiyo.
Malecela alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa na
gazeti hili kutoa maoni yake kuhusu mgogoro wa kusafirisha gesi kutoka
mkoani Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam unaoendelea kushika kasi
katika siku za hivi karibuni.
“Ukiwa karibu na waridi unatakiwa kunukia waridi. Wakazi wa Mtwara nao wanatakiwa wanukie waridi,” alisema.
“Ukiwa karibu na waridi unatakiwa kunukia waridi. Wakazi wa Mtwara nao wanatakiwa wanukie waridi,” alisema.
Malecela alisema, pamoja na ukweli kwamba
rasilimali inayopatikana nchini ni kwa ajili ya watanzania wote, ukweli
kwamba wakazi wa eneo inakopatikana rasiliamali hiyo wanapaswa kunufaika
nayo, haukwepeki.
“Hatutakiwi kuwaacha hivi hivi wana-Mtwara eti kwa
sababu hii ni rasilimali ya Watanzania wote. Ni lazima wanufaike zaidi,
wao kuliko wengine kwa kuwa wako karibu na waridi,” alisema Malecela.
Alisema licha ya gesi hiyo kuwa ya watanzania wote, Serikali inatakiwa kuandaa utaratibu ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Mtwara wananufaika zaidi na rasilimali hiyo.
Alisema licha ya gesi hiyo kuwa ya watanzania wote, Serikali inatakiwa kuandaa utaratibu ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Mtwara wananufaika zaidi na rasilimali hiyo.
Malecela alieleza kuwa umaskini uliokithiri katika
baadhi ya mikoa nchini ukiwamo mkoa wa Mtwara, ndio unaosababisha watu
waanze kudai rasilimali zinazotoka katika maeneo yao wakiamini kuwa ndio
mwanzo wa ukombozi wao.
“Serikali iyaangalie kwa umakini maeneo yanayotoa utajiri na rasilimali, ni lazima wapewe upendeleo ili wafurahie matunda mali asili yao,” alisema Malecela.
“Serikali iyaangalie kwa umakini maeneo yanayotoa utajiri na rasilimali, ni lazima wapewe upendeleo ili wafurahie matunda mali asili yao,” alisema Malecela.
Kuhusu gesi kutoka Mtwara
Malecela alisema anaunga mkono gesi kusafirishwa mahali popote palipo na soko kubwa ili iweze kuwanufaisha Watanzania lakini, lazima kuwe na mkakati wa kuwanufaisha pia wakazi wa eneo husika.
“Mnaweza kuisafirisha gesi kwenda mahali popote
palipo na soko kubwa, lakini mkaangalia namna mnavyoweza kuwanufaisha
wakazi wa Mtwara,” alisema na kuendelea;
“Rasilimali inayogundulika popote ndani ya Tanzania ni mali ya watanzania wote, hivyo hata gesi ya Mtwara si ya wakazi wa Mtwara peke yao.”
“Rasilimali inayogundulika popote ndani ya Tanzania ni mali ya watanzania wote, hivyo hata gesi ya Mtwara si ya wakazi wa Mtwara peke yao.”
“Kama ilivyo kwa bwawa lililopo katika Jimbo la
Mtera linalozalisha umeme na kuingizwa katika gridi ya taifa kwa ajili
ya watanzania wote, gesi nayo inatakiwa kuwanufaisha watanzania wote,”
Mkazi Mtwara atishia gesi kutoonekana
Katika hatua nyingine Kikongwe Somoe Issa (90) ambaye ni mkuu wa kaya ya Msimbati, kijiji ambacho gesi asilia inavunwa ameionya Serikali kutoendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi.
Katika hatua nyingine Kikongwe Somoe Issa (90) ambaye ni mkuu wa kaya ya Msimbati, kijiji ambacho gesi asilia inavunwa ameionya Serikali kutoendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi.
Kikongwe huyo ambaye haoni wala kusikia alisema
hayupo tayari kuona gesi hiyo ambayo imepatikana katika kijiji hicho
ikiondoka mkoani Mtwara.
“Atakayejaribu kuondoa gesi hii kitakachomkuta
atakijua yeye mweyewe…ninasema gesi isiende kokote…iwapo atabisha
inawezekana akasafirisha maji tu na isiwe gesi yenyewe” alisema bibi
huyo kupitia kwa mkalimani wake Asha Hamis
Aliongeza kuwa,“mwaka walioanza kuchimba (2005)
walifika hapa bila kubisha hodi, wanajua kilichowakuta…bomba lilikuwa
haliendi chini wala kurudi juu…walinifuata hapa nikaenda kufanya
tambiko”
MWANANCHI
Bibi huyo alilazimika kutumia lugha ya kimakonde kwa maelezo
ndiyo anayoifahamu vizuri, alisema wakati wa tambiko hilo wazungu
waliokuwa katika mradi huo walilazimika kunywa maji kwa kutumia kifuu
cha nazi ambapo mmoja wao alikataa.
“Yule aliyekataa niliwaambia aondoke, wale wenzake
walimsafirisha na baada ya hapo waliaza kuchimba na gesi ikapatika…leo
wanasema gesi inaondoka, hilo sikubali…mimi ndiye mwenye eneo hili,
nilifanya tambiko gesi ipatikane na sasa nitafanya tambiko isiondoke”
alisisitiza kikongwe huyo ambaye hajui mwaka aliozaliwa.
Kauli ya Kikongwe huyo kupinga gesi kwenda Dar es
Salaam na kutishia kusafirishwa kwa maji badala ya gesi iwapo serikali
itapuuza madai ya wananchi inarejesha historia ya vita ya Majimaji
iliyoasisiwa wilayani Kilwa, mkoani Lindi mwaka 1905-7.
Katika vita hiyo viongozi wa kimila walisema kuwa
bunduki za wazungu zitatoa maji badala ya risasi, jambo ambalo
lilihamsisha wananchi wengi kupigana vita hivyo.
Kwa kauli hiyo ya mkuu huyo wa kaya anaungana na
wakazi wengi wa Mkoa wa Mtwara wanaopinga mradi huo, wakiwemo wanasiasa,
viongozi wa dini, mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji na CCM wilaya
ya Mtwara mjini.
Katika salamu zake za mwaka mpya, Rais Kikwete,
alisema gesi ni mali ya Watanzania lakini akasema Serikali itahakikisha
inaandaa utaratibu kwa wananchi wa Mtwara kunufaika zaidi na gesi hiyo.
Hivi karibuni wananchi wa Mtwara waliandaa maandamano kupinga usafirishaji wa gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Sakata hilo lilizikidi kuchukua sura mpya baada ya
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Mikindani, Mtwara,
Ali Chinkawene na Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM) Hasnain Murji kumpinga
Rais Kikwete wakitaka gesi isisafirishwe kutoka Mtwara kwenda Dar es
Salaam.
MWANANCHI



No comments:
Post a Comment