HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MBUNGE ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI HUKU AKINYESHEWA NA MVUA



Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe (pichani)akubali kunyeshewa na mvua kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Chanjale wilayani Ludewa ambao walikuwa wakilalamikia ufisadi unaofanywa na viongozi wao wa kijiji na kata.

Mbunge huyo ambae awali kabla ya kuanza kuwahutubia wananchi alipewa mwamvuli kwa ajili ya kujikinga na mvua iliyoanza kunyesha muda mfupi kabla ya kuanza kuwahutubia wananchi hao ,baadae alikataa kujifunika mwamvuli huo kwa madai kuwa hawezi kujifunika mwamvuli kula starehe wakati wananchi wake wanakero na wananyeshewa na mvua.

 Kutokana na hali hiyo mbunge huyo aliendelea kusikiliza na kujibu maswali mbali mbali ya wananchi juu ya ufisadi unaofanywa na viongozi wa kata hiyo kwa kushindwa kusoma mapato na matumizi wala kuitisha mkutano kijijini hapo.
 Wananchi hao mbali ya kumpongeza mbunge huyo kwa kuonyesha mfano kwa viongozi wengine kwa kufika kulala katika kijiji hicho na kusikiliza kero zao ,bado walisema kuwa viongozi wa kijiji hicho na kata wamekuwa ni tatizo kubwa na wao kama wananchi wameonyesha kuwachoka viongozi hao.
 Akizungumza katika mkutano huo mbunge Filikunjombe alisema kuwa anasikitishwa na utendaji wa viongozi wa kata hiyo kwa kushindwa kufanyia kazi matatizo ya wananchi wa kijiji hicho hata kwa kushindwa  kujenga  choo cha wanafunzi .

Hata  hivyo alisema kuwa ofisi yake anachukua hatua ya kuchangia  kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya  kusaidia ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika shule ya Msingi Chanjale

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: