Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana kuunga mkono wakazi wa Mtwara kupinga
usafirishaji wa gesi kwenda Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Kampeni na
Uchaguzi NCCR, Faustine Sungura. Picha na Michael Jamson
ASEMA HERI AFUKUZWE KULIKO KUIONA
IKISAFIRISHWA, MWENYEKITI WA CCM NAYE APIGILIA MSUMARI, MREMA, MBATIA
WAWAUNGA MKONO, DC ATAKA ELIMU KWANZA
MBUNGE wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji na
Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Mikindani, Ali Chinkawene wamepinga kauli
ya Rais Jakaya Kikwete kwamba wakazi wa Mkoa wa Mtwara hawapaswi kuzuia
gesi kwenda Dar es Salaam.
Juzi, katika salamu zake za Mwaka Mpya, Rais
Kikwete alipinga madai ya wakazi wa Mikoa ya Kusini kutaka gesi hiyo
isisafirishwe kwenda Dar es Salaam, akisema madai hayo hayakubaliki
popote.
“Rasilimali inayopatikana popote katika nchi hii
ni mali ya taifa zima na hutumika kwa manufaa ya taifa na katu si mali
ya watu wa pale ilipogundulika au pale shughuli inapofanyika,” alisema
Rais Kikwete.
Viongozi hao mbali na kuonyesha misimamo ya kuzuia
nishati hiyo hata kabla ya kauli hiyo ya Rais Kikwete, jana
walisisitiza kwa nyakati tofauti kwamba, wataendelea kuunga mkono
jitihada za wananchi kupinga usafirishwaji wake kwa kuwa hiyo ni haki
yao.
Murji alisema yupo tayari kuvuliwa ubunge kwa
kutetea masilahi ya Wanamtwara wanaopinga gesi hiyo inayovunwa katika
Kijiji cha Msimbati, mkoani Mtwara huku Chinkawene akisema msimamo wa
chama chake ni kuungana na wananchi kupinga gesi kupelekwa Dar es
Salaam.
Alisema Serikali inapaswa kujenga mitambo ya
kuzalisha umeme mkoani Mtwara badala ya Dar es Salaam... “Tulipoona hali
inakuwa tete, niliitisha kikao cha Kamati ya Siasa kujadili nini
msimamo wa chama katika hili. Kamati ya Siasa wakasema hawawezi
kukisemea chama kwa sababu chama ni wanachama, hivyo nikaitisha kikao
cha Halmashauri Kuu ambapo pia tuliwaalika mabalozi wa mitaa.”
“Katika kikao hicho, wajumbe walipinga kwa nguvu
zote suala la gesi kupelekwa Dar es Salaam. Wakaniambia niseme msimamo
wao kuwa hawataki gesi iende Dar es Salaam hadi pale masilahi ya
Wanamtwara yatakapowekwa wazi na Serikali.”
Mwenyekiti huyo alisema kwa maana hiyo, msimamo
huo si wake binafsi, bali ni maazimio ya vikao halali vya chama hicho
vinavyowakilisha wanachama na kwamba historia ya Mikoa ya Kusini jinsi
ilivyonyimwa maendeleo ilitumiwa na wajumbe kujenga hoja hiyo.
“Wakati sisi hatuna umeme hakuna aliyefirikia
kutuunganisha kwenye gridi ya Taifa… Barabara ya kutoka Mtwara kwenda
Dar es Salaam miaka 51 ya Uhuru sasa, haijakamilika. Lakini bomba
wanataka kujenga kwa miezi 18. Hivi kuna Watanzania muhimu zaidi ya
wengine?” alihoji Chinkawene akinukuu kauli za wajumbe wa kikao hicho na
kuongeza:
“Walizungumza mambo mengi, suala la kung’olewa kwa
reli, kukatazwa kulima pamba, kuuawa kwa kilimo cha karanga na mkonge.
Haya yote wanadai yamesababisha mkoa uendelee kuwa maskini na kwamba
tumaini lao limebaki kwenye gesi. Wamesema wapo pamoja na wananchi.”
Murji kwa upande wake, alisema amekutana na umoja
wa vyama vya siasa vilivyoratibu maandamano ya kupinga suala hilo na
kuwapongeza kwa kazi nzuri akisema wananchi wana haki ya kutetea
rasilimali yao.
Alisema yeye si mbunge anayewakilisha mawazo yake bungeni, bali ya wananchi... “Hivyo ni bora niungane na wananchi wangu kutetea masilahi yao; liwalo na liwe.”
Alisema yeye si mbunge anayewakilisha mawazo yake bungeni, bali ya wananchi... “Hivyo ni bora niungane na wananchi wangu kutetea masilahi yao; liwalo na liwe.”
“Nawapongeza viongozi wa vyama vya siasa kwa
ujasiri na uthubutu wenu wa kutetea rasilimali hii (gesi)… Tusidharau
hata kidogo malalamiko ya wananchi…” alisema Murji huku akishangiliwa na
wajumbe na kuongeza:
“Nipo pamoja nanyi na hata ikibidi nivue ubunge, nipo tayari kufanya hivyo kwa masilahi ya wananchi….”
“Nipo pamoja nanyi na hata ikibidi nivue ubunge, nipo tayari kufanya hivyo kwa masilahi ya wananchi….”
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile alisema si sahihi
kuwalaumu wananchi wanaopinga kupelekwa kwa gesi hiyo Dar es Salaam kwa
kuwa hawajaelimishwa.
“Ni kweli hatuwezi kueleweka kama gesi inakwenda
Dar es Salaam wakati hawajui watanufaikaje. Hayo si maswali madogo,
lazima yajibiwe,” alisema alipokuwa akifungua Baraza la Majadiliano
baina ya uongozi na vyama vya wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara mwishoni
mwa wiki.
Alipoulizwa jana kama amefuta kauli yake hiyo hata
baada ya Rais Kikwete kutoa mwongozo wake alijibu: “Nilisema ni muhimu
wananchi waelimishwe, wasilaumiwe tu, kwani wameelimishwa tayari?… Hata
Rais (Kikwete) hajakataa kuelimisha.”
Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Uledi Abdallah
ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mtwara Mjini, alimpongeza
mbunge huyo kwa kuungana na wananchi hao na kuahidi kumpa ushirikiano
huku akisisitiza kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kutanguliza
masilahi ya wengi.
“Tumefarijika kuona wenzetu wa CCM na wewe mbunge
wetu umeungana na sisi…. Tofauti zetu za kisiasa tuziweke kando,
tusimamie rasilimali yetu,” alisema Uledi.
Mbunge wa Vunjo (TLP), Agustine Mrema ameunga mkono harakati za wakazi hao wa Mikoa ya Kusini kushinikiza gesi isisafirishwe kwenda Dar es Salaam akisema wana haki ya kudai maendeleo katika maeneo yao kwanza.
Mbunge wa Vunjo (TLP), Agustine Mrema ameunga mkono harakati za wakazi hao wa Mikoa ya Kusini kushinikiza gesi isisafirishwe kwenda Dar es Salaam akisema wana haki ya kudai maendeleo katika maeneo yao kwanza.
“Si kwamba wakazi hao ni wachoyo, hapana wamechoka
ni kama Mungu amewaamsha katika usingizi, sasa wanataka haki yao,”
alisema Mrema.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema
wananchi wa Mtwara na Lindi wana haki ya kuhoji jinsi watakavyonufaika
na gesi kwa sababu baadhi ya viongozi wa Tanzania wana tabia ya kutaka
kujinufaisha wao kwanza.
“Baada ya wananchi kuibua hoja kuhusu gesi, baadhi
ya viongozi wa Serikali wameibuka na kuwaita wahaini, kauli hizi
zinaweza kuligawa taifa, kila mwananchi ana haki ya kuhoji juu ya
rasilimali za taifa,” alisema.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John
Mnyika ameitaka Serikali kueleza matumizi ya mapato yanayotokana na gesi
iliyogundulika katika Mkoa wa Mtwara tangu mwaka 2004 ili wananchi
waweze kufahamu wananufaika vipi na rasilimali hiyo.
Mnyika alisema madai ya wakazi wa mikoa hiyo kupinga gesi isisafirishwe kwenda Dar es Salaam ni ya msingi kwani hawaoni faida yake.
Mnyika alisema madai ya wakazi wa mikoa hiyo kupinga gesi isisafirishwe kwenda Dar es Salaam ni ya msingi kwani hawaoni faida yake.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo alisema madai hayo ni mwanzo wa kuimega nchi vipandevipande kwa
faida ya wachache.
“Hii si gesi yao, ni ya Watanzania wote, hatupaswi
kuanza kuimega nchi katika vipande kwani kila eneo lenye maendeleo
halijayapata kivyakevyake, bali ni mpangilio na mgawanyo bora wa
rasilimali,” alisema.
Mbunge wa Masasi Mjini (CCM), Mariam Kasembe
alisema anaungana na Rais Kikwete kupinga madai ya wakazi wa Kusini na
kusema kuwa gesi kupelekwa Dar es Salaam si kigezo cha maeneo hayo
kukosa maendeleo.
Habari hii imeandikwa na Abdallah Bakari (Mtwara), Florence Majani, Fidelis Butahe na Aidan Mhando (Dar).
MWANANCHI
Wiki
iliyopita, Umoja wa vyama vya siasa mkoani Mtwara uliitisha maandamano
kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam, wakitaka ibaki mkoani
humo kwa faida ya wakazi wake. Umoja huo ambao awali ulikuwa ni wa vyama
vinane vya Chadema, NCCR-Mageuzi, SAU, TLP, APPT Maendeleo, ADC, VDP na
DP, sasa unaungwa mkono na CCM na CUF.
Habari hii imeandikwa na Abdallah Bakari (Mtwara), Florence Majani, Fidelis Butahe na Aidan Mhando (Dar).
MWANANCHI



No comments:
Post a Comment