Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akimkabidhi Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Aggrey Mwanri Vitabu vya Mafanikio ya Miaka 50
ya Uhuru Mkoa wa Rukwa mara baada ya kuvizindua katika moja ya matukio
ya shughuli zake za kikazi mkoani Rukwa. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa
wa Katavi Mhe. Dkt. Rajab Rutegwe.
………………………………………………………….
NA KIBADA KIBADA WA FULLSHANGWE-KATAVI
Watumishi wote wa umma wametakiwa
kuwajibika vyema katika maeneo yao ya kazi na kila mmoja kwa nafasi
yake katika utoaji wa huduma pale alipo ili kuleta maendeleo
yanayokusudiwa kwa ujenzi wa Taifa.
Akizungumza katika kikao cha
majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano idara ya Maji
Wilayani mpanda Mkoani Katavi mara baada ya kumaliza ziara yake katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Wilaya ya Mlele Naibu waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri alihimiza
uwajibikaji na utendaji kazi mzuri kwa kila mtumishi wa umma na kila
mtu kwa nafasi yake katika jamii iwapo atatimiza wajibu ataweza
kufanikisha suala la kuleta maendeleo kwa Taifa na yeye Mwenyewe.
Amesema uzalendo ni muhimu sana
katika utendaji wa Kazi bila uzalendo katika kazi hakuna mafanikio,
mataifa yote yaliyofanikiwa kiuchumi ni kutokana na uzalendo wa watu
wake kuipenda nchi na kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili
kufikia mafanikio waliyojiwekea.
Alisema watumishi wanatakiwa
wachape kazi kwelikweli ili iwe mfano kwa wananchi wengine katika maeneo
wanaokofanyia huduma ya utumishi wao,wajitume kwa nguvu zote.
Amesema serikali ina miundo mbinu
mizuri sana iwapo wananchi wote wangekuwa na uzalendo wa kuisimamia
kwa pamoja na kufanya kazi kwa nguvu kwa kujituma bila kusukumwa Taifa
lingepiga hatua kubwa ya maendeleo.
Katika ziara yake wilayani mpanda
na Mlele ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa lengo la kuona
fedha zinazoletwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya miradi ya maendeleo
kama zinasimamiwa vizuri,na miradi iliyotekelezwa inalingana na thamani
ya fedha yenyewe iliyotolewa na serikali kuu.
CHANZO: FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment