HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Dk Mwinyi akiri upungufu wa dawa za malaria nchini

 
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk Hussein Mwinyi. 
 
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk Hussein Mwinyi amesema dawa za ugonjwa wa malaria za Alu, hazikupatikana kutokana na matatizo ya mitambo inayotumika kuzitengeneza lakini sasa zipo.

Waziri Mwinyi aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kugawa vifaa vya kujimudu kwa watu wenye ulemavu vyenye thamani ya Sh500 milioni.
Alisema dawa hizo zinanunuliwa na Serikali na zinaingizwa kwa msaada wa Taasisi ya Global Fund.

Dk Mwinyi alilazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia taarifa za vituo 1,300 nchini, kutokuwa na dawa hizo.
Taarifa zilizokuwa zikinukuliwa na Taasisi ya Sikika kupitia mtandao wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, zilidai asilimia 25 ya vituo havikuwa na dawa hizo tangu Januari mwaka huu.

Kwa upande wa vifaa ambavyo wizara yake imegawa, Dk Mwinyi alisema serikali imenunua vifaa hivyo kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii, ili kuwezesha wazee na walemavu kumudu maisha yao.“Napenda kuwasihi watakaopata vifaa hivi wasivitumie kwa biashara au kuviuza, wavitunze vizuri kwa kujua kuna watu wengine wenye ulemavu ambao wanavihitaji,” alisema Dk Mwinyi na kuongeza:

“Lakini kulingana na uwezo wa Serikali hatukuweza kuwapatia wote kwa pamoja.” Alisema wizara inatoa huduma kwa vyuo vitano vya watu wenye ulemavu na makazi 17 ya wazee.
“Serikali inatoa huduma za chakula, matibabu, elimu, vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika vyuo hivyo na huduma za utengamano, nyenzo za kujimudu na ushauri nasaha,” alisema.

Baadhi ya vifaa vilivyogawiwa jana ni bajaji 10, baiskeli za walemavu 30 na vitanda vya chuma 117.



MWANANCHI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: