MTOTO mchanga hivi karibuni ametupwa katika Mto Kikundi mjini hapa akiwa
amekufa, jirani kabisa na kambi ya makahaba wanaofanya biashara ya
kuuza miili yao ‘machangudoa’. Baadhi ya watu walioshuhudia mwili wa
kichanga hicho walimwambia mwandishi wetu kuwa kichanga hicho kilitupwa
na mmoja wa makahaba, hali iliyozua tafrani kwani wasichana wanaoaminika
kuwa ni makahaba walikuwa wakiipinga kauli hiyo.
“We mpigapicha usiamini hayo wanayosema hao watu... tuna ujinga kiasi gani tuzae, tuue kisha tutupe mtoto sehemu yetu ya kazi?” alihoji msichana mmoja ambaye alikataa kujitambulisha.
Hata hivyo, wasichana waliojitambulisha kwa majina Pendo Komba, Rose Joseph na Amanda Athuman kwa nyakati tofauti walisema wanaofanya unyama huo ni makahaba japokuwa wenyewe wanakataa.
Walidai kuwa hii ni mara ya sita kwa watoto wachanga kutupwa kwenye eneo hilo.
Afisi mmoja wa polisi aliyekuwepo eneo hilo, (jina tunalihifadhi) wakati wanauchukua mwili wa kichanga hicho alisema wanamtafuta mwanamke aliyefanya ukatili huo ili afikishwe mahakamani.

No comments:
Post a Comment