MADHARA YA KUVAA VIATU VYENYE VISIGINO VIREFU
KULINGANA na utafiti uliofanywa hivi karibuni na wataalamu wa magonjwa
ya miguu kwa binadamu, imebainika kuwa watu wengi huwa wanazaliwa wakiwa
hawana matatizo ya miguu. Hata hivyo, kwa kupuuza taratibu za kiafya na
ushauri wa wataalamu, watu wengi hupata magonjwa ya miguu wakiwa watu
wazima. Taarifa hiyo inazidi kueleza kuwa, kundi lililopo kwenye hatari
kubwa ni wanawake ambao inakadiriwa kuwa wanasumbuliwa na matatizo ya
miguu, mara nne zaidi ya wanaume.
Wanawake huwa katika hatari kubwa kutokana na mazoea ya kuvaa viatu
vyenye visigino virefu. Inaelezwa kuwa asilimia 90 ya wanawake
wanaofanyiwa upasuaji mdogo au mkubwa wa miguu, huwa ni kwa sababu ya
uvaaji wa viatu usiozingatia kanuni za afya kwa kuvaa viatu vyenye
visigino virefu.
Sababu za wanawake kuvaa viatu vyenye visigino virefu, ni kutaka
waonekane warefu, wawe na mvuto zaidi na kwenda na fasheni. Licha ya
sababu hizo, uvaaji wa viatu vyenye visigino virefu (kuanzia inchi 2)
huwa na madhara makubwa kuliko faida.
Kulingana na utafiti wa kitaalamu, mwanamke wa kawaida ana uwezo wa
kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku. Visigino virefu hufanya nguvu
inayotumika kutembea hatua moja kuwa kubwa kuliko kawaida, huku
vikimnyima raha ya kutembea kwa uhuru.
Visigino virefu huhamisha uzito wa mwili kutoka kwenye visigino vya
miguu mpaka kwenye magoti, mapaja na kiuno, na nguvu kubwa inayotumika
huishia katika viungio vya mifupa (balls and socket) na kusababisha viwe
vinasuguana na kuleta maumivu.
Kwa kawaida, miguu ya binadamu, hasa visigino, vimeumbwa ili kuutegemeza
uzito wa mwili juu ya ardhi. Uvaaji wa viatu virefu hufanya uzito wa
mwili kubebwa na kisigino kirefu, hivyo uzito wa mwili kushindwa
kusawazika.
Matokeo yake husababisha misuli na mishipa ya miguu, kiuno, mgongo na
shingo kufanya kazi kubwa ya kujaribu kusawazisha uzito, kazi ambayo kwa
kawaida hufanywa na visigino. Hii husababisha miguu, kiuno, na mgongo
kuwa katika hatari kubwa ya kupatwa na matatizo ya kiafya, ikiwemo
kuteguka na kuvunjika.
Visigino virefu hubadili muundo wa mifupa ya miguu, hivyo kusababisha
magoti na misuli ya mapaja (tendons) kufanya kazi ya ziada ili kuupa
mwili balansi. Kwa kuwa misuli inakuwa inafanya kazi kubwa, uwezekano wa
kupatwa na maumivu makali ya miguu na kushindwa kutembea katika siku za
baadae huwa mkubwa.
Visigino virefu husababisha maumivu ya visigino, damu kuvilia ndani ya
miguu, mpangilio wa mifupa ya vidole kuvurugika, mishipa na misuli ya
tendon kuwa mifupi, neva za fahamu kufungana na kushindwa kufanya kazi
yake. Tatizo huendelea kwa vifundo vya miguu (ankle) , magoti, na mifupa
ya kwenye mapaja kushindwa kujivuta na kulegea (stretch and relax) na
hivyo kusuguana wakati wa kutembea, hali ambayo kama haikudhibitiwa
mapema, madhara yake huwa ni makubwa kwa siku za baadaye.
Hatua/Steps za kufuata:
- Anza na viatu virefu kiasi inchi 2 - 3 na ukiweza kuvimudu unaenda ukiongeza urefu wake, usijaribu kutoka kutokuwahi kuvaa viatu virefu na kuanza na vile virefu labda vya inchi nne na zaidi ni hatari na hutaweza kumudu. Hii itasaidia kuizoesha miguu yako kupata nguvu ya kutembelea viatu virefu.
- Ukiweza kumudu mfano wa viatu hapo juu anza na vile vyenye urefu kiasi / kitten heels ili uweze kuizoeza miguu yako kuwa na balance ya kutosha
Post a Comment