Wananchi wa Mtaa wa Igodima kata ya Iganzo, Mbeya waandamana
Wakazi zaidi
ya 50 wameandamana hadi katika Ofisi za kata ya Iganzo wakidai kupewa
eneo la kufanyia biashara huku wakiwa na majembe wakimtaka mweshimiwa
diwani wa kata hiyo awagawie eneo hilo kwani wamechoka kudaganywa mara
kwa mara
Ni vurugu tupu
Diwani Uswege Furika (Chadema) kata ya Iganzo akiwatuliza wakazi wake watulie ili awaeleze ukweli kilichotokea
Kiukweli mambo yote anayafahamu yulee yaani akimnyooshea afisa mtendaji
wa kata hiyo kuwa anafahamu vyema juu ya kiwanja hicho cha soko
Wananchi wangu sasa sijui tufanyeje maana naona hili swala limekuwa gumu
kwangu itabidi nikae na uongozi wangu halafu nitawapa jibu
Mweshimiwa diwani tunataka haki yetu
Mweshimiwa diwani twende eneo la tukio ukatupatie maeneo yetu tuanza
biashara tunaomba sana baba huyo dada akimsihi mweshimiwa diwani
Mbona hamnielewi nimewaambia ngoja nikae na viongozi wenzangu tuwashughulikie swala lenu mweeeee
Wakazi wa Iganzo baada ya kuone hawamweliwi diwani wao wakaamua kuondoka
kueleea kwenye kwenye eneo walilotakiwa kupewa ili wakajigawie wenyewe
maeneo yao
Haooo wanaondoka
Mweshimiwa diwani haamini macho yake anapoona wananchi wake wanaondoka bila ya kumsikiliza
Hili ndilo eneo walilotakiwa kugawiwa sasa wananchi hao wanachagu uongozi wao wa muda ili waanza kujigawia eneo hilo
HILI NDILO ENEO WANANCHI HAWA WATAJIGAWIA WENYEWE KWA AJILI YA SOKO BAADA YA MWESHIMIWA DIWANI KUWADANGANYA (Habari na picha na Mbeya Yetu)
WAKAZI wa Mtaa wa Igodima kata ya Iganzo Jijini Mbeya wameandamana
kushinikiza kutekelezewa ahadi walioahidiwa na Diwani wa Kata hiyo ya
kuwagawia eneo kwa ajili ya kufanyia biashara.
Wakazi hao zaidi ya 50 wameandamana hadi katika Ofisi za kata na
kupokelewa na uongozi wa kata hiyo akiwemo Diwani Uswege Furika
(Chadema) na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Jumapili Mwasenga huku wakiwa
na majembe mikononi wakishinikiza kuanza kugawiwa eneo hilo.
Awali ilidaiwa kuwa Diwani huyo aliwaahidi wananchi hao kuwapa eneo kwa
ajili ya biashara ambapo aliwaambia wananchi hao kufika eneo husika
asubuhi mapema kwa ajili ya kila mtu kuoneshwa sehemu yake ambayo
angefanyia biashara zake.
Aidha katika hali isiyokuwa ya kawaida Diwani huyo alipingana na
wananchi hali iliyozua mzozo mkali baina yake na wananchi ambapo
alikataa kutoa ahadi hiyo lakini baada ya kubanwa sana alikubali na
kudai kuwa suala hilo alilifikisha kwa Ofisa Mtendaji wa Kata.
Baada ya Ofisa mtendaji kupewa nafasi ya kulizungusuala hilo pia
alipingana na Diwani huyo kwa madai kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa
juu ya ahadi hiyo hivyo alichokifanya Diwani huyo alipotosha wananchi.
Ofisa huyo Jumapili Mwasenga alisema suala la Wnanchi kudai eneo la Soko
ni madai ya msingi lakini yana taratibu zake namna ya kuyapata kuongeza
kuwa kama Diwani aliahidi alitakiwa kutoa taarifa Ofisini kwake ili
walifanyie utaratibu.
Aliongeza kuwa pamoja na ahadi hiyo bado yeye kama Mtendaji anatekeleza
Ilani ya Chama cha Mapinduzi na siyo Chama kingine hivyo Diwani alipaswa
kupeleka maombi ya wananchi kwa maandishi ili yafanyiwe kazi.
Kufuatia majibu hayo yaliyoibua hasira kali kwa wananchi ambao walianza
kupiga kelele wakidai kuoneshwa eneo ili wakaanze kupanga meza tayari
kwa biashara ambapo Mtendaji huyo aliwaahidi wananchi kusubiri ili
taratibu zianze kufanyika ili wapewe eneo hilo.
Wananchi hao hawakulizika na majibu ya Mtendaji huyo hali iliyopelekea
kumbana Diwani wakidai kuwa hawana imani naye kwa kuwa alikurupuka kutoa
ahadi huku akifahamu utaratibu unaotakiwa kufuatwa kabla ya kuanzishwa
kwa soko.
Godfrey Sanga mkazi wa Mtaa wa Igodima alisema Suala la maendeleo ya
kata ya Iganzo limekuwa likipigwa danadana kila siku ambapo Diwani
kupitia mkutano wa chama cha Chadema uliofanyika Jumapili iliyopita
aliwaahidi wananchi hao kuwa wafike kwa ajili ya kupewa maeneo hali
iliwalazimu wananchi kufika eneo hilo wakiwa na majembe mikononi.
“ Wanatuona kama watoto tusiokuwa na akili huyu diwani yeye mwenyewe
aliahidi kututengenezea barabara na soko alisema lipo eneo tayari sisi
tuje ili kila mtu apewe sehemu yake lakini badala yake anatugeuka”
alihoji Hassan Kasangula mkazi wa mtaa wa Igodima.
Hata hivyo wananchi hao walionesha kutoridhika na kauli za viongozi hao
hali iliyowalazimu kufika eneo la soko na kuchagua uongozi wa mpito na
kuanza kujigawia tayari kwa kuanza biashara huku uongozi ukibaki
unashangaa.
Aidha kufuatia hali hiyo Diwani huyo alimtupia lawama Mwenyekiti wa
Chadema wa kata hiyo kuwa ndiye aliyetoa ahadi hiyo kwenye mkutano hali
iliyosababisha yeye kulaumiwa na wananchi akihusiashwa na ahadi hiyo.
Post a Comment