HAYA NI MAJINA MENGINE YA AJIRA MPYA YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU MWAKA 2012/2013 YALIYOTOLEWA TAREHE 27/02/2013


Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imefanya mapitio ya orodha ya walimu wa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu iliyotangazwa tarehe 13/02/2013. Baada ya mapitio hayo, walimu wote wenye masomo ya kufundisha sekondari ambao walikuwa wameachwa, sasa wamepangwa. Walimu ambao hawana somo la kufundisha katika shule za sekondari hawakupangwa.

Walimu waliopangwa wanatakiwa kuripoti ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na Vyuo vya ualimu wakiwa na vyeti halisi vya taaluma na cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake ifikapo Machi 01, 2013. Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo Machi 09, 2013 atapoteza nafasi hiyo na hatapata fursa ya kuajiriwa tena.

Aidha, Wizara inawakumbusha Walimu ambao walikuwa wameajiriwa na Serikali kabla ya kwenda masomoni kurudi katika vituo vyao vya kazi. Walimu watakaokiuka watachukuliwa hatua za kinidhamu na waajiri wao.

Tangazo hili limetolewa na:
Katibu mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
27/02/2013

icon Orodha ya Walimu wa Shahada 2013 (1.38 MB)

icon Orodha ya Walimu wa Stashahada 2013 (658.7 kB)

icon Orodha ya Wakufunzi na Walimu wa Shule za Mazoezi za Sekondari 2013 (35.84 kB)

No comments

Powered by Blogger.