HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Airtel yazindua gharama nafuu zakupiga simu mitandao mingine

picture 1Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel  Bi, Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma mpya  ya Airtel Yatosha inayomwenzesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi , sms na internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, huduma hii imebeba ujumbe wa  simkadi moja, taifa moja, bei moja
picture 2
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akielezea huduma mpya ya Airtel yatosha  yaani Simu kadi moja, taifa moja, bei moja inayomwezesha mteja wa Airtel kuwasiliana na mitandao yoyote nchi na kupata kifurushi cha muda wa maongezi, sms, na internet kwa bei nafuu hadi shiling 349/= pichani (katikati) ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel  Bi, Beatrice Singano Mallya akifatiwa na Meneja masoko Airtel Anethy Muga Sunil Colaso MD Airtel jpg (1)
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel yatosha inayomwezesha mteja wa Airtel kupata dakika za muda wa maongezi,sms na kifurushi cha internet.

*Piga simu muda wowote usiku and mchana
Dar Es Salaam  Jumatano 20 Marchi 2012.  Airtel Tanzania leo imezindua huduma mpya ijulikanayo kama “AIRTEL YATOSHA” itakayowawezesha wateja wake  nchi nzima kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa kiwango nafuu cha hadi asilimia 75 bila kuwa na  sababu kubadili simu laini kwa kuhofia gharama.
Huduma ya AIRTEL YATOSHA inadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei moja  inayoendeleza dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora na nafuu ambapo wateja wa Airtel sasa watapata ofa ya kifurushi kitakacho wapa muda wa maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet ambacho kinaweza kutumika kwa siku au kwa wiki kulingana na mahitaji ya wateja.
Akiongea wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa huduma hiyo iliofanyika katika makao makuu ya Airtel Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw Sunil Colaso Alisema”  Huduma ya Airtel YATOSHA ni maalum kwa kila mtanzania, hii itawarahisishia watanzania wote kupata mawasilino nafuu kwa kupiga bila kikomo kwenda mitandao mingine nchini. Kupitia kifurushi cha Airtel YATOSHA wateja wa Airtel watafurahia kiwango cha chini cha hadi shilingi 349/=, hii inamaana kwamba  mteja atapata dakika 10 za kupiga simu kwenda mtandao wowote muda wowote, pia SMS 100 (ujumbe mfupi wa maneno) pamoja na kifurushi cha intenet cha 25MB ofa itakayotumika masaa 24 kwa siku
Faida za AIRTEL YATOSHA kwa mteja zinadhihirisha dhamira yetu Airtel ya kutoa huduma za mawasiliano bora na nafuu nchini. Airtel tunazingatia kuwa wateja wetu wanamahitaji tofauti na ndio sababu kubwa inayotufanya tuwe wabunifu kwa kuwapatia huduma zinazogusa kila aina ya wateja na kuleta mabadiliko halisi kwa kuwapa wateja wetu nchi
nzima thamani ya pesa zao

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: