Nyota wa Ugiriki, Giorgos Katidis
ATHENS, UGIRIKI
NYOTA wa Ugiriki, Giorgos Katidis amefungiwa kutocheza soka maisha yake yote baada ya kuonyesha saluti ya Nazi, lakini mwenyewe amejitetea kwa kusema alishangilia bila kujua maana ya ishara hiyo.
Kiungo huyo wa AEK Athens mwenye miaka 20, alionyesha ushara hiyo wakati akishangilia bao lake la ushindi kwenye mchezo dhidi ya Veria Jumamosi iliyopita.
Shirikisho la Soka la Ugiriki limesema kuwa limeamua kumfungia mchezaji huyo kwa kuwa aliwatukana watu wote ambao waliwahi kupata madhara ya saluti hiyo.
"Mimi si fashisti, nisingetoa ishara hiyo kama ningeelewa maana yake," alisema Katidis katika mtandao wa Twitter.

Mchezaji huyo ambaye ni nahodha wa zamani wa timu
ya Ugiriki ya vijana wa chini ya miaka 19 alilalamikiwa kwa kutoa
saluti hiyo baada ya kufunga bao la ushindi kwenye mchezo ambao
ulimalizika kwa AEK kushinda mabao 2-1 dhidi ya Veria kwenye Uwanja wa
Olimpiki.
Alisema alikuwa akimwonyesha kidole mchezaji mwenzake aliyekuwa jukwaani.
Lakini klabu imemtaka mchezaji huyo ajieleze kwa kina kwenye mkutano wa bodi wiki ijayo.
Saluti ya kinazi ilikuwa ikitumika enzi za utawala wa Adolf Hitler ambapo watu wa kawaida na wanajeshi walikuwa wakilazimika kunyoosha mikono kumsalimu dikteta huyo ambaye alikuwa akijulikana duniani kote kwa ukatili wa kibinadamu. Saluti hiyo ilitumika mpaka mwaka 1944 wakati Hitler alipofariki.
Tangu wakati huo mpaka sasa salamu hiyo imepigwa marufuku katika nchi za Ujerumani, Austria na Jamuhuri ya Czech. Mtu yeyote anayetoa ishara hiyo hupewa adhabu kali.

MWANASPORT

No comments:
Post a Comment