KIJANA AMKATA SHOKA MAMA YAKE MZAZI MPAKA KUFA MOROGORO
Frank
Hillary, 27, aliyetambuliwa kuwa mlokole, amethubutu na kuweza
kukatisha maisha ya mama yake, Ndolukasi Lugamo, 50, akitumia shoka
kuondoa uhai wa mzazi wake.KWELI kuelekea mwisho wa dunia, mengi yataonekana. Mtu unawezaje kumpiga
shoka mama yako mzazi, aliyekutunza tumboni mwake kwa miezi tisa,
akakunyonyesha, kukusomesha hadi kukua na kujitegemea?
Tukio
zima, lilichukua nafasi Alhamisi iliyopita, Mtaa wa Malipula, Kata ya
Chamwino, mkoani Morogoro na inadaiwa kwamba kabla ya mauaji, Hillary
alimpiga vibao, mitama na mateke mama yake.(Picha na Mpekuzi)
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Pili Athuman, alidai kwamba siku ya tukio, kulitokea mabishano kati ya Hillary na mama yake.
“Yalikuwa mabishano kidogo lakini ghafla yule kijana alimvamia mama yake na kuanza kumpiga,” alisema Pili na kuongeza:
“Yule kijana ni mtoto wa pekee wa yule mama. Tunashindwa kuelewa mpaka sasa chanzo cha tukio hilo. Halafu wale watu ni walokole kabisa na siku zote walikuwa wanaishi kwa upendo.”

Shuhuda
mwingine, Julius Josephat alisema: “Mimi nashindwa kuelewa. Huyu
marehemu na mwanaye walikuwa wanapendana sana, wakienda kanisani
wanaongozana kama kumbikumbi.
“Kinachosikitisha zaidi ni kuwa mama yake aliumia mkono kama siku tatu kabla, akawa amefungwa plasta ngumu (POP), nahisi ndiyo maana alishindwa kujiokoa.”

Naye
Maria Maswika ambaye nyumba yake imepakana na ile ya mama Hillary,
alieleza: “Leo (Alhamisi), saa 4 asubuhi nilimsikia huyo mama akipiga
kelele za kuomba msada, huku akiingia nyumbani kwangu.
“Nilipotoka chumbani, nilishuhudia kwa macho yangu yule kijana akimpiga shoka mama yake na kumuua palepale. Sababu ya ugomvi wao siielewi. Kwanza nashangaa sana, kwani yule mama wa watu alikuwa anampenda sana mtoto wake.”
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio mapema na kushuhudia wananchi wakimkamata Hillary, kumfunga kamba kabla ya polisi nao kuwasili, kuandika maelezo na kumchukua mtuhumiwa huyo wa mauaji ya mama yake mzazi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustine Shilogile, alisema: “Uchunguzi zaidi wa tukio unaendelea na utakapokamilika, tutamfikisha mtuhumiwa mahakamani.”

Kitu kilichowashangaza wengi eneo la tukio ni paka anayetajwa
kumilikiwa na marehemu ambaye baada ya mama huyo kuuawa, yeye alikwenda
kulamba damu kisha akalala kichwani kwenye mwili wa marehemu.
Post a Comment