Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Ultimate Security wakiendelea kuzima
moto uliokuwa ukiendelea kuwaka ndani ya ghala hilo,ambao tayari
ulikwisha teketeza mali nyingi. (Picha na Vijimambo Blog)
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka ndani ya ghala hilo kama uonekanavyo pichani.
Moto mkubwa umezuka na kuteketeza mali mbalimbali zilizokuwemo kwenye
moja ya ghala kubwa la kuhifadhia vitu mbalimbali ikiwemo vikombe vya
udongo,Pampas,vigae na vitu vingine,sehemu ya maghala ya kuhifadhia vitu
Shekilango,jijini Dar,aidha kufuatia tukio hilo mpaka Globu ya Jamii
inaondoka eneo la tukio,hasala naa gharama za mali zilizoteketea
haikuweza kufahamika mara moja,aidha kwa mujibu wa Kamanda wa mkoa wa
Kipolisi Wilaya ya Kinondoni,Afande Kenyela alieleza kuwa mpaka sasa
chanzo cha moto huo bado hakijafahamika isipokuwa juhudi za kuuzima moto
zilikuwa zikiendelea kwa juhudi kubwa.






No comments:
Post a Comment