HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MWALIMU BERNADETA MINJA AMEFARIKI KWA AJARI YA BASI LA MOHAMED TRANS USIKU WA JUMAPILI

 
 Marehemu Bernadeta Minja Enzi za Uhai Wake

Mwalimu Bernadeta Minja wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Idara ya Uchumi na Biashara Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) amefariki dunia jana usiku katika ajali ya basi la Mohamed iliyotokea juzi usiku eneo la Gairo akiwa safarini kuelekea Dodoma yeye pamoja na mtoto wake mwenye miezi sita (6) na mfanyakazi wake wa ndani na watu wengine 11 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya Muhamed Trans likitokea Dar es salaam kwenda Dodoma baada ya kupata ajali katika eneo la Kiegea, Gairo barabara ya Morogoro Dodoma . Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi wakati akijaribu kupita lori lililoharibika.
 
  Marehemu Bernadeta Minja, MA, PhD candidate (Economics)

Nimeweka picha zake kutoka Facebook page yake (http://www.facebook.com/bernadeta.minja ) kuweka sura badala ya kuwa ni takwimu tu, ili iwaguse watu. Huyu dada alikua ni mmojawapo wa future ya nchi yetu. Young lady ambaye alikua ni PhD candidate, na lecturer wa Economics katika chuo kikuu anapoteza maisha kirahisi hivi sababu ya upumbavu wa baadhi ya madereva, na vyombo vya sheria barabarani ambavyo neno “kuwajibika” halipo katika misamiati yao. Marehemu Bernadeta alikua na mtoto wake mwenye umri wa miezi mitano ambaye ni mmoja wa majeruhi kwenye ajali hiyo.
 

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina la bwana libarikiwe

PAMOJAPURE BLOG INATOA POLE KWA FAMILIA, UONGOZI WA UDOM, WALIMU WA UDOM NA MARAFIKI WA BERNADETA MINJA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: