Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa
ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo
lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi
Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa
kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi
zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo
hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti
wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na
mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi
saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali
hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na
wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa
watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa
limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia
Ithnaasheri. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata
maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw.
Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la
jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam asubuhi
saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali
hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na
wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa
watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa
limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia
Ithnaasheri.
Raisi Jakaya Kikwete Akiangalia
Jinsi zoezi la Uokoaji linavyoendelea mara baada ya kuwasili kwenye eneo
la tukio katika Mtaa wa Zanaki na Hindra Ghandi
Wananchi wakiendelea na zoezi la uokoaji katika eneo la tukio mapema ya leo
Baadhi ya wakazi wa jiji la dar
wakifunga minyororo kwenye moja ya kontena lililofukiwa na vifusi baada
ya jengo la ghorofa 15 kuporomoka
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakiwa katika zoezi la uokoaji
Madaktari wa kujitolea wakimhudumia mmoja wa majeruhi waliyeokolewa kwenye ghorofa lililopolomoka leo asubuhi.
Usalama uliimarishwa kila kona ya eneo la tukio huku askari wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi wakifanya kazi yao ipasavyo
Askari wakifanya kazi yao kuhakikisha usalama unakuepo
Wananchi wakiendelea na zoezi la kuondoa kifusi kwaajili ya kuokoa watu waliofukiwa na vifusi
Gari likitolewa baada ya kuangukiwa na vifusi mara baada ya jengo la ghorofa 15 kuanguka
Vijana Wa JKT wakiendelea na zoezi la uokoaji katika eneo la tukio
Askari wa Jeshi la Polisi na Wananchi wakibadilishana mawazo kuhakikisha zoezi linaenda vizuri
Zoezi la Uokoaji likienda huku greda zikifanya kazi ya kusomba vifusi
Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia zoezi la uokoaji kutoka Vikosi vya Uokoaji na wananchi waliojitolea kuokoa uhai wa wenzetu.
PICHA NI KWA HISANI YA LUKAZA BLOG
PICHA NI KWA HISANI YA LUKAZA BLOG







No comments:
Post a Comment