HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » RAIS KIKWETE ATEMBELEA TENA ENEO LA TUKIO WAKATI ZOEZI LA UOKOAJI LIKIENDELEA

 Eneo la tukio ambapo jengo la ghorofa zaidi ya 10 liliporomoka jana asubuhi na hadi kufikia saa sita mchana leo maiti 18 zilikuwa zimeopolewa na watu wanne wakiwemo wakandarasi waliokuwa wanajenga pamoja na wahandisi wa halmashauri ya wilaya ya Ilala wanashikiliwa na polisi, wakati wawili wanaendelea kusakwa ikiwa ni pamoja na mjenzi ambaye kapewa masaa 12 kujisalimisha. Kuna habari kwamba jengo hilo refu kulia pia linajengwa na mkararasi aliyejenga hili lililoporomoka na kila aliye sehemu hii analiangalia kwa jicho la wasiwasi.(Picha na Full Shangwe)
 Rais Kikwete akiwa eneo la tukio tena leo, baada ya kutembelea jana,  akitoa maagizo kwa Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova kwamba kila aliyehusika na ujenzi wa jengo hilo kuanzia mchoraji, msimamizi na mjenzi wahojiwe na wawajibishwe wakipatikana na kosa 
 Rais Kikwete akiongea na viongozi wa msikiti wa Shia ithnaasheri wakati anaondoka eneo la tukio


Mkuu wa Polisi Kanda Maalum Mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika eneo la Tukio kwenye jengo lililoanguka jana maeneo ya Posta jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu, Majeruhi na  Uharibifu wa mali, Mpaka mchana huu imethibitika ni watu 20 wamenasuliwa kutoka  katika  kifusi cha jengo hilo na majeruhi kadhaa, kazi ya uutafuta miili ya watu waliopoteza maisha inaendelea mpaka sasa katika eneo hilo huku vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na taasisi mbalimbali vinashirikiana kwa pamoja kuhakikisha vinakamilisha kazi ya kutafuta miili ya watu waliopoteza maisha katika trukio hilo. 2
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi  CUF Profesa Ibrahim Lipumba akihojiwa na mwandishi wa habari wa TBC Grace Kingalame wakati alipotembelea eneo la tukio na kujionea hali halisi ya uokoaji. 3 
Kazi ya kukata nondo ili kuondoa kifusi hicho ikiendelea  4
Mashine za kuondoa kifusi zikiwa zinaendelea na zoezi hilo. 5  
 
 
11
 
  12

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: