HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » RICH ONE ASHUKIWA KUMTAPELI STAMINA

 Rich One
  
Ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu msanii Rich One kusemekana kutapeli pesa kwa promota akidai yeye ndio Ally kiba na kuchukua pesa kwa njia isiyo halali, jana kupitia u head ya xxl, amesikika rapper Stamina akimshutumu Rich one kwa kutaka kuchukua hela za show kutoka kwa promota alietaka aende kufanya show Kahama na wasanii aliokuwa anawataka promota huyo ni Dayna, Kitale na Stamina na kikubwa alichokisema Stamina alisema yeye anamuachia mungu tu maana Rich One amefikia kutaperi hata yeye kiukweli imemuuma na kumuona kaka yake amekuwatapeli kwa wasanii wenzie. 

Promota alikuwa hana namba ya Stamina ila alikuwa anajuana na Rich One ndipo alipomtumia ili aweze kupata namba ya Stamina. Kilichofuta ni Rich One kumpa Promota huyo wa Kahama namba feki ya Stamina na kuanza kuongea nae huyo Stamina feki na namba yake ilikuwa inaishia na 89. Na pia Rich One alifikia kuzungumzia masuala ya malipo ya stamina kama ataenda kufanya shoo huko kahama atalipwa shilingi laki saba 700,000/= za kitanzania ambazo Stamina alikuwa hakuusishwa kwa namna yoyote.

Rich One alidai kuongea na Stamina na kudai anamjua sana Stamina ndipo kumpa namba ya Stamina feki napia promota aliambiwa na Rich one suala la Stamina amwachie yeye atamaliza kila kitu., baada ya promota kushuku kuwa Stamina anaeongea nae sio kwa kuwa alikua akisisitiza sana kutumiwa hela ya advance, ndipo aliamua kujaribu kuomba namba ya Stamina kwa muigizaji Kitale na alipopewa aliona ni namba tofauti na aliyokuwa amepewa na Rich One, ndipo alipoamua kufanya mawasiliano na Stamina wa ukweli. 
 Stamina
Pia Kitale alimpigia Stamina kumjulisha suala lake la kutaka kutapeliwa na Rich One kwa kutaka kupiga mpunga kutoka kwa promota huyo wa Kahama ndipo Kitale akamsisitiza Stamina ampigie simu Promota ili ajue habari kamili. Stamina alipoongea na promota huyo kwa simu promota alimuuliza Stamina kama ndo yeye maana alikuwa ametengenezwa Stamina feki ili kupiga mpunga. Promota huyo aliweza kumtumia Stamina wa ukweli sms alizokuwa anatumiwa na Stamina fefi zikisisitiza kutoa advance. Pia Rich One alishamtaperi promota huyo ndio maana alikuwa anatafuta namba ya Stamina wa ukweli.

Stamina amesema wameongea na huyo Promota wamekubaliana kwenda kufanya shoo ila Stamina kamsisitiza Promota siku nyingine hawe makini na mataperi kama Rich One. Hivi kama Stamina ameweza kugundua mchezo mchafu aliokuwa anataka kuchezewa na kaka mkubwa Rich One je ni wangapi wametapeliwa pesa zao? Maana hata ishu ya Ali Kiba ni kama hii ya Stamina aliyokuwa anataka kuliwa pesa zake bure.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: