Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria
wa Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) Steve Kilindo akimkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya sh. mil. 60, Diwani wa Kata ya Sasilo wilayani
Manyoni, mkoani Singida, Robert Mussa kwa ajili ya uchimbaji wa visima
vya maji 20 ili kupunguza tatizo la maji. Wanaoshuhudia tukio hilo
lililofanyika juzi katika kata hiyo ni Meneja wa TBL Kanda ya Kusini,
James Bokela (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Manyoni, Fortunata Malya. (Picha na Full Shangwe)
Wananchi wa kata ya Sasilo
wilayani Manyoni Mkoa wa Singida wakifurahia baada ya kata hiyo
Kukabidhiwa hundi ya Tsh 60 Mil iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania
[TBL] kwa ajili ya uchimbaji wa visima 20 vya maji ambapo waliomba
kupiga nayo picha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida, Fortunata Malya akitoa shukrani kwa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa kutoa msaada wa sh. mil 60 katika
Kata ya Sasilo kwa ajili ya uchimbaji wa visima 20 vya maji. Hafla ya
makabidhiano ilifanyika hivi karibuni katika kata hiyo.
Mkazi wa Kijiji Cha Sasilo
Wilayani Manyoni Mkoa wa Singida Selebia Robert 51 mfugaji akiwa
Nyumbani kwake pamoja na Familia yake kwenye pozi la picha huku wakiwa
na vibuyu vya kuchotea maji na matumaini ya kupata maji Baada ya Kata
yao kukabidhiwa Milion 60 na TBL kwa ajili ya Uchimbaji wa visima 20 vya
maji vitakavyopunguza tatizo Hilo.
Meneja wa kampuni ya Bia Tanzania
[TBL] Kanda ya Kusini, James Bokela akizungumza na wananchi wa Kata ya
Sasilo, wilayani Manyoni, baada ya hivi karibuni kampuni hiyo kukabidhi
msaada wa sh. mil 60 za kusaidia kuchimba visima vya maji.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria
wa Kampuni ya Bia Tanzania [TBL] Steve Kilindo akifafanua jambo mbele ya
wananchi wa kata hiyo wakati alipoenda kukabidhi msaada wa 60 milion
kwa ajili ya Uchimbaji wa Visima 20 vya maji.
Wananchi wa kata ya Sasilo
wakifuatilia jambo wakati walipokuwa wakishuhudia upokeaji wa Msaada wa
Tsh 60 mil zilizotolewa na TBL kwa ajili ya uchimbaji wa visima vya maji
20 makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Selakari ya mtaa na
Mtendaji



No comments:
Post a Comment