Jana usiku, kampuni ya Magazeti ya Mwananchi Communications ilizindua
muonekano mpya wa gazeti lake la Mwananchi ambapo ilifanya halfa fupi
katika ukumbi wa Mlimani City, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbali
mbali wa kiserikali, vyama vya siasa, wafanyabiashara, wadau wa habari
na watu mbali mbali maarufu jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na
Mwenyekiti wa Tume yamarekebisho ya Katiba, Balozi Joseph Sinde Warioba.
Pichani juu anaonekana Mheshimiwa Warioba(Wa pili kutoka kushoto,
akishiriki katika zoezi la uzinduzi wa gazeti hilo lenye muonekano mpya,
pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo, Bi Zuhura Muro, huku
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw Tido Mhando(kushoto), na Meneja
Biashara na maendeleo, Bw Theophil Makunga(kulia) wakishuhudia. (PICHA NA VIJIMAMBO)
Mhariri Mtendaji wa kwanza wa gazeti la Mwananchi, ambaye kwa sasa ni
Meneja Maendeleo yaBiashara akieleza kwa kina kuhusiana na miaka 13 ya
Gazeti la Mwananchi na mafanikio yake kwa waalikwa
Nasaha kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bw Tido Mhando
Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari, Dk Reginald
Mengi, Mgeni Rasmi Mh Warioba, na Mwenyekiti wa Bodi wa MCL Bi Zuhura
Muro wakiteta jambo
Mwenyekiti wa Bodi naye alisema machache
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la mwananchi, Bw Dennis Msacky(kulia), akiwa
na Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya MCL, Bakari Machumu na mtaalam
wa ubunifu wa kurasa Bi Kelly Frankeny
Uzinduzi rasmi.
Huu ndio muonekano mpya!
Linapendeza kwa kweli
Umeona mwenyewe, hapa ni kila sehemu ya ndani imefanyiwa marekebisho
Picha na watu mashuhuri
Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma kaskazini pamoja na katibu mwenezi wa Chama Cha mapinduzi, Nape Nnauye wakiteta jambo
MCL Team
Meza kuu ilipata nafasi ya kuperuzi, ...na kudadisi...
Baadae kila mtu alipata nakala yake
Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari, Dk Reginald Mengi akitoa nasaha zake
kelly Frankey, mtaalamu wa miundo mbali mbali ya gazeti la mwananchi naye alipata wasaa wa kujieleza mbele ya wageni waalikwa
Kila mtu alifurahi
Mshereheshaji alikuwa Taji Liundi, moja kati ta wakongwe katika tasnia ya utangazaji
Baada ya yote, Skylight Band ikamaliza mambo kwa burudani ya Nguvu



No comments:
Post a Comment