Mkufunzi maarufu sana aliyewahi kupata mafanikio makubwa nchini
Uingereza, Sir Alex Ferguson atajiuzulu kama kocha wa klabu ya
Manchester United mwishoni mwa msimu huu wa 2012/2013
Ferguson alishinda mataji 13 ya Ligi kuu ya soka England wakati wa
uongozi wake wa misimu 26 katika klabu hiyo. Klabu imetoa taarifa leo
iliyomnukuu Ferguson akifafanua kuwa msimu huu wa 26 ndio utakaokuwa
wake wa mwisho. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 71 amesema ametafakari
sana kuhusu uamuzi wa kustaafu kwake.
Amesema ameonelea ni muhimu kuondoka katika klabu hiyo wakati ikiwa katika hali nzuri na anaamini ametimiza hilo. Fergie amewapokonya Manchester City taji la Premier Legaue msimu huu na kulirejesha katika uwanja wa Old Trafford ikiwa ni taji la 20 la klabu hiyo. Kocha huyo ambaye sasa atasalia kama mkurugenzi mkuu na mjumbe wa klabu ya Manchester United, amesema ana matumaini kuwa amejiuzulu kama mkufunzi wakati klabu hiyo ikiwa katika hali nzuri kabisa.
Nani atakayemrithi Fergie?
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho, ambaye aliweka uhusiano mzuri wa utani wakati alipokuwa kocha wa mahasimu wa United, Chelsea, pia amepigiwa upatu kupewa nafasi hiyo.
David Gill ambaye aliweka ushirikiano wa kiwango cha juu cha mafanikio na Fregie kama Afisa Mkuu Mtendaji ikiwa ni pamoja na ushindi wa mataji matatu katika msimu mmoja wa mwaka 1999 – Premier League, Champions League na Kombe la FA, amepeana salamu za pongezi na heri njema kwa kocha huyo.
Amesema imekwua heshima kubwa na furaha yeye kufanya kazi na Alex kwa takribani miaka 16, kipindi ambacho mataji mengi yamewekwa kabatini.
Ferguson anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mfupa wa nyonga mwishoni mwa msimu huu lakini kabla ya uvumi kuanzishwa jana Jumanne, hakukuwa na dalili kuwa angejiuzulu.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu
SOURCE:DW
Amesema ameonelea ni muhimu kuondoka katika klabu hiyo wakati ikiwa katika hali nzuri na anaamini ametimiza hilo. Fergie amewapokonya Manchester City taji la Premier Legaue msimu huu na kulirejesha katika uwanja wa Old Trafford ikiwa ni taji la 20 la klabu hiyo. Kocha huyo ambaye sasa atasalia kama mkurugenzi mkuu na mjumbe wa klabu ya Manchester United, amesema ana matumaini kuwa amejiuzulu kama mkufunzi wakati klabu hiyo ikiwa katika hali nzuri kabisa.
Nani atakayemrithi Fergie?
Sir Alex Ferguson aliiongoza Manchester United kutwaa taji la 20 la Premier League mwezi Aprili
United hawajatoa dalili zozote za ni nani atakayevivaa viatu
vya Sir Alex Ferguson wakati kukiwa na uvumi kuwa meneja wa Everton
David Moyes huenda akaijaza nafasi hiyo ya katika uwanja wa Old
Trafford.Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho, ambaye aliweka uhusiano mzuri wa utani wakati alipokuwa kocha wa mahasimu wa United, Chelsea, pia amepigiwa upatu kupewa nafasi hiyo.
David Gill ambaye aliweka ushirikiano wa kiwango cha juu cha mafanikio na Fregie kama Afisa Mkuu Mtendaji ikiwa ni pamoja na ushindi wa mataji matatu katika msimu mmoja wa mwaka 1999 – Premier League, Champions League na Kombe la FA, amepeana salamu za pongezi na heri njema kwa kocha huyo.
Amesema imekwua heshima kubwa na furaha yeye kufanya kazi na Alex kwa takribani miaka 16, kipindi ambacho mataji mengi yamewekwa kabatini.
Ferguson anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mfupa wa nyonga mwishoni mwa msimu huu lakini kabla ya uvumi kuanzishwa jana Jumanne, hakukuwa na dalili kuwa angejiuzulu.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu
SOURCE:DW

No comments:
Post a Comment