katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya,
Wiliamu Simwale alifika ofisi ya Mbeya yetu na kuanza kumsikiliza Amina (Picha na Mbeya yetu)
KATIKA
Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo
Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu
kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina.
Mwanafunzi
huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa
ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka
huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi
wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa tukio
hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa jambo hilo na
kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura mitaani asijue hatma
ya maisha yake.
Mhanga
wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na
wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali
iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi
asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo
za kujisitiri kama Shuka nk.
Anasema
kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua
yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo baada ya kukosa msaada
ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.
Binti
huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun iliyoko Jijini Dar Es
Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku akiomba
msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya
kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
Kwa
upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu
kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha mwanafunzi
huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi wenzie na kuongeza
kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.
Naye
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alisema
alikuwa halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti
angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea
kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika
linalolipa.
Mlezi
wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume amesema
kwamba hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa
anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya kilichotokea
ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka ili Mwanafunzi
aendelee na masomo kama kawaida.
|
No comments:
Post a Comment