MSANII
mkongwe wa filamu Bongo, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ aligongwa na
gari wakati akifanya mazoezi ya kutembea kufuatia ugonjwa wake wa
kiharusi.
Tukio
hilo lilitokea Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Kariakoo, Dar ambapo gari
hilo aina ya Toyota Voxy lilitokea ghafla na kumgonga kidogo na
kumsababishia michubuko miguuni na kichwani.
Dereva wa gari hilo alifanya
uungwana kwa kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi ambapo ndugu
zake walitaarifiwa na kwenda kumchukua.
“Mzee Kankaa alitoka nyumbani
na kuwaaga kuwa anakwenda kufanya matembezi. Walijua ni karibu, lakini
baadaye tukasikia taarifa kuwa amepata ajali na yupo Kituo cha Polisi
Msimbazi,” alisema Abdul ambaye ni mtoto wa Kankaa.Kuangalia mzee kama huyu katangaza sana kazi ya sanaa ya Tanzana lakini saizi hali yake sio nzuri au tunasubilia siku yaza msiba kuonesha ufahari wa kutoa michango pamoja na kuuza sura. Wengi wamefanyiwa hivyo sasa tubadilike Watanzania wenzangu.
No comments:
Post a Comment