Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akisalimiana kitabu cha kampeni ya
Lishe Tanzania baada ya kukizindua leo Machi 16, 2013 katika bustani ya
Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali
Hassan Mwinyi na kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria
Nyerere(Picha na Ikulu)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha kampeni ya Lishe Tanzania
baada ya kukizindua leo Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja
jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Peniel Lyimo akifuatiwa na
Mkurugenzi wa kwanza wa Taasisi ya Chakula na Lishe Mzee Lema. Kushoto
ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere
Mama
Maria Nyerere akifurahia tuzo maalumu aliyopokea kwa niaba ya Baba wa
Taifa aliyotunukiwa na Taasisi ya Chakula na Lishe kwa mchango wake
mkubwa kwa kukuza na kuendeleza sera ya lishe nchini wakati wa sherehe
za uzinduzi wa Kampeni ya Lishe Tanzania leo Machi 16, 2013 katika
bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
tuzo maalum iliyotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe kutambua mchango
wake mkubwa katika kusimamia lishe na maendeleo yake nchini katika
uzinduzi wa kampeni ya lishe nchini leo Machi 16, 2013 katika bustani
ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali
Hassan Mwinyi na kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria
Nyerere
No comments:
Post a Comment