Kutumika pia kama sehemu ya
kuomboleza msiba wa Ngwea na kushirikisha wakali kibao kama vile Mb Dog, Madee,
Diamond, Nay wa Mitego na wengineo
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
ONYESHO kubwa ambalo ni uzinduzi
wa Shindano la QS Queens linalotarajiwa kufanyika Jumamosi ya kesho ya Juni
Mosi katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala, pia limepangwa kuwa sehemu maalum ya
kuenzi mchango wa msanii Albert Mangwea, aliyefariki nchini Afrika Kusini.
Diam0nd
kushoto na Ney wa Mitego kulia kumenyana tena katika Ukumbi wa Dar Live
Jumamosi, Mb Dog, Madee, Juma Nature na wengine kibaaao.
Ngwea amepangwa kuletwa kesho
Jumamosi kwa ajili ya maziko yake yaliyopangwa kufanyika mkoani Morogoro, huku
onyesho hilo la maombolezo likihudhuliwa na wakali kibao wa muziki hapa nchini
lilioandaliwa kwa muda mrefu na kilele chake kuwa Jumamosi hii.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, leo mchana, Meneja Masoko wa Kampuni
ya QS Mhonda J Entertainment, Freddy Felix, alisema kuwa shindano hilo
litafanyika pia katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata warembo 20
watakaoishi katika Jumba moja kwa ajili ya kupata kimwana huyo wa QS Queens.
Alisema kuwa wasanii wengi
wamepangwa kupanda jukwaani kwa ajili ya kuomboleza msiba huo, akiwamo Ney wa
Mitego, Wanaume Halisi, ikiongozwa na Juma Nature, MB Dog, Diamond, Inspector
Haroun, Madee, H-Baba, Snura, Khadija Kopa, Solid Ground Family na wengineo,
wakiwamo wasanii chipukizi, Amor na Shalviny.
“Wasichana wote wanaotaka
kushiriki shindano hili ambao ni kama uzinduzi wake, watajiandikisha katika
fomu maalum ukumbini hapo, ambapo baadaye watatafutwa wengine ambao wote
wataishi kwa miezi miwili katika nyumba moja itakayotembelewa na watu
mbalimbali.
“Huku mshindi akijishindia gari
la kifahari, pia wanapokuwa katika jumba hilo kila siku mtu atalipwa kadri
tutakavyokubaliana, huku tukiamini kuwa huu utakuwa ni mwanzo mzuri katika
shindano hili,” alisema Felix.
Kwa mujibu wa Felix, shindano
hili kabla ya kupatikana warembo hao litatembelea mikoa kadhaa ya Tanzania
Bara, kama vile Mwanza, Tanga, Morogoro, Mbeya, Iringa na kwingineko kwa ajili
ya kutafuta msichana mmoja wa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.
Aidha QS ilitangaza kuwa
mabinti wanaotakiwa kushiriki katika shindano hilo ni wale wenye vipaji maalum
na uwezo wowote wa kupambanua mambo, huku kigezo cha elimu kikiwekwa pembeni.
Shindano hilo pia litaonyeshwa
katika vituo vya Channel Ten, DTV, Clouds, ambapo huko kote wadau na wapenzi wa
mambo ya urembo na burudani watapata fursa ya kuwapigia kura washiriki kabla ya
siku ya kilele chake kitakachofanyika baadaye mwaka huu.
No comments:
Post a Comment