Kijana anayedaiwa kuwa
tapeli akiwa mikononi mwa raia.
Kwa muda mrefu kumekuwa na
malalamiko kuhusu uwepo wa jamaa anayedaiwa ni tapeli aarufu Dar kisha kuingia
mzigoni na kumnasa ‘laivu’ ambapo alihenyeshwa kwa kibano cha karne na raia
waliokuwa na hasira.Mtego huo ulifyatuka Jumanne ya Mei 21, mwaka
huu ambapo kijana mmoja (jina halikupatikana) alinaswa na kupewa ‘henyahenya’
ya aina yake huku akinusurika kuchomwa moto.
Bila kujua kuna mtego, kijana huyo aliingia kwa
mbwembwe katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar na kukaa katika
moja ya viti kisha kuita mhudumu na kuchomoa noti ya shilingi ‘buku’ kumi,
akaagiza misosi.Akiwa amemeza tonge moja tu, aligeuka akatazama mlangoni,
akamuona jamaa mmoja akimfuata kwa mwendo wa kasi na katika hali ya taharuki,
ndipo akakurupuka akitaka kutoka nduki.
Jamaa akiendelea
kuhenyeshwa na wananchi.
ILIKUWAJE?
Majira ya saa 9:00
alasiri, ghafla kijana huyo aliibua tafrani alipokurupuka mbio kutoka nje ya
ukumbi huo.Nyuma ya kijana huyo,
jamaa aliyekuwa amedaiwa kutapeliwa na mtu huyo alianza kumkimbiza akipiga
kelele za mwizi ndipo baadhi ya raia nao wakaanza kumfukuzia.
Baada ya kichapo jamaa
alivishwa tairi tayari kupigwa kiberiti.
ATIWA MIKONONI
Raia hao walitimua
mbio wakimfukuza kijana huyo na walipofika maeneo ya Vijana, Kinondoni,
kwa bahati mbaya alijikwaa na kuanguka ndipo akatiwa mikononi.Yule jamaa ambaye
alikuwa anamwitia mwizi, alikuja mbio na kuwaambia watu kuwa huyo ni tapeli
ambaye alimtapeli shilingi laki tatu na nusu baada ya kumsomesha kuwa yeye ni
mwajiri wa kampuni moja.Aliyetapeliwa alidai
kuwa katika utapeli huo, kijana huyo huwa anashirikiana na mzee mmoja ambaye
huwa anavaa nguo nadhifu huku akiwa anatembea na ‘briefcase’ mkononi. Baadhi ya picha
alizokutwa nazo tapeli huyo.
Jamaa huyo ‘aliposachiwa’
alikutwa na vitu kibao vya kitapeli yakiwemo makaratasi yaliyokatwa na kufungwa
kwa noti bandia za shilingi elfu kumi zinazoonekana kama burungutu la fedha
kumbe hakuna chochote ni ‘bosheni’.Pia alikutwa na vitambulisho kibao vya watu vikiwemo vya kupigia kura, leseni
na picha za ‘passport size’ za watu mbalimbali.Katika makabrasha yake
kulikutwa barua mbalimbali za serikali za mitaa za jijini Dar.Alipoulizwa kuwa vitu
hivyo vya watu na nyaraka za serikali ni vya nini au alivipataje, jamaa huyo alijitetea
kuwa ana mtu anayeshirikiana naye katika michongo hiyo.
Jamaa akiwa ameiva
baada ya kichapo.
APEWA KIBANO CHA KARNE
Baadaye wananchi wenye
hasira kali walichukua sheria mkononi na kumpa kibano huku akitakiwa kumpigia
simu bosi wake aje eneo hilo.
Zoezi la kuja kwa bosi
wake lilishindikana baada ya kupigiwa simu na kumkana hivyo baadhi ya watu
walimvisha tairi la gari wakamwagia mafuta ya petrol, tayari kwa kumchoma moto.
Baadhi ya vitambulisho
alivyokutwa navyo tapeli huyo.
Huku akiwa amehenyeshwa kwa kipigo na kulowa damu chapachapa, wakitaka kumchoma
moto, madereva teksi wa eneo la Vijana, Kinondoni waliwakataza wasimchomee
maeneo hayo kwani hawakutaka ushahidi hivyo wakamwachia akiwa nyang’anyang’a.
PICHA NA MDODOSOAJI
No comments:
Post a Comment