Wagonjwa
walioathirika na bomu la kurushwa jumapili iliyopita wakiwa
wanapandishwa kwenye gari ya wagonjwa tayari kwa kupelekwa katika
kiwanja kidogo cha ndege cha mkoa Arusha kwa ajili ya kuamishiwa katika
hospitali ya muhimbili jijini dar es salaam. Mahmoud Ahmad Arusha.Picha
na Woinde Shizza.
Mtoto
akiwa amebebwa na baba yake huku akipokelewa na nesi wa hospitali ya
Mount Meru kwa ajili ya kupelekwa kiwanja cha ndege cha Arusha kwa ajili
ya kusafirishwa kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Mmuhimbili
jijini Dar es Salaam kwa matibabu
Wagonjwa walioathirika na bomu la kurushwa jumapili iliyopita wakiwa wanapandishwa kwenye gari ya wagonjwa tayari kwa kupelekwa katika kiwanja kidogo cha ndege cha mkoa Arusha kwa ajili ya kuamishiwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam
Na Mahmoud Ahmad Arusha
Wagonjwa
saba ambao ni majeruhi wa mlipuko wa bomu kwenye kanisa la Joseph
Mfanyakazi eneo la Olasiti jijini Arusha wamehamishiwa kwenye Hospitali
za Muhimbili na LUgalo jijini Dar es Salaam.
Majeruhi
hao wamesafirishwa mchana majira ya saa tisa kwa ndege ya shirika la
Hifadhi za taifa (TANAPA) kwenda kuendelea na matibabu zaidi baada ya
hali zao kuonekana bado zinahitaji vifaa vyenye uwezo wa hali ya juu.
Miongoni
mwa walisafirishwa wapo watoto watatu wakike wawili na wakiume mmoja
huu wakina mama walisafirishwa wakiwa wawili na kinababa wawili ambao
hali zao bado mbaya licha ya matibabu walikuwa wakiyapata tokea juzi.
Wasamaria
wema kutoka makampuni mbali mbali wameendelea kutoa misaada mbali mbali
ya hali na mali ikiwemo madawa na vifaa tiba na mablanketi na
mashuka,na Magodoro iliviisaidie hospitali za Mt.Meru na St,Elizabeth.
wakati
huo huo wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wamewatembelea
wahanga wa bomu na kutembelea kanisa ambalo yalitokea maafa na kujionea
hali halisi wakiongozwa na spika wa bunge hilo Anna Makinda
Miongoni
mwa wabunge hao ni Mh.Habibu Mnyaa ambaye alisema kuwa hali kama hiyo
imewatia simanzi na kuiomba serekali kuchukuwa tahadhari kubwa kwa
matukio kama haya akiongea mbunge wa viti maalumu ccm vijana Catherine
Maggige alsema kuwa majeruhi hawa wanatia huruma na kuwa kitendo hicho
kilichotokea hakliwezi kuvumilika na kuiomba serekeli kuchukuwa hatua za
haraka kukabiliana na wimbi la tukio kama hilo.
Kwa
upande wake spika makinda hakuweza kutoa neno lolote bali aliingia
kweny Gari teyari kwa safari ya kurudi Dodoma huku akiwa na huzuni
kubwa.
No comments:
Post a Comment