Omba omba tapeli anayejifanya hana mikono akikamatwa na wananchi baada ya kukimbia
Wananchi eneo la Miyomboni wakiwa wamembana omba omba huyu tapeli kuonyesha mikono yake yote
'' Huwa unasema wewe ni mlemavu huna mkono mmoja hii nini ....nyosha juu watu waone utapeli wako"
Hapa ni kipigo kikiendelea
Tapeli huyo akitaka kujinasua kutoka mikono ya wananchi wenye hasira kali
Hapa baada ya kupata upenyo akivaa nguo zake
Hapa akiwa ameachiwa na kuanza kutimua mbio
Baada ya kuchezea kichapo tapeli huyo sasa anajaribu kuficha aibu
OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO KWENYE TUKIO LA KWANZA
Huyu ni omba omba anayeigiza kutokuwa
na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri kuomba
chochote kutoka kwa wapita njia leo
Hapa akisubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema leo
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera ya mtandao huu leo
AMA Kweli mwisho wa utapeli ni aibu
kubwa na wahenga walinena kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya
filauni leo kwa wakazi wa Miyomboni mjini Iringa wamepata kushuhudia
kituko cha mwaka baada ya watu waliochoka kuvumilia vitendo vya
kitapeli vinavyofanywa mzee mmoha ambae amekuwa akiigiza ni mlemavu
asiye na mguu mmoja na mkono mmoja.
Tapeli huyo mbali ya kuumbuliwa kwa
kutakiwa kuonyesha miguu yake yote pamoja na mikono yake yote
bado amepata kuchezea kichapo kiasi cha kunusurika kuuwawa na
wananchi hao wenye hasira kali.
Tukio la mzee huyo kubainika kama ni tapeli kwa mara ya kwanza mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com ndio ulipata kufichua siri hiyo ya omba omba huyo kuwa si omba omba kutokana na kumnasa akijiweka mfano wa mlemavu .
Kutokana na kufichuliwa kwa siri hiyo
ya kujiigiza kuwa ni omba omba mlemavu wananchi wamekuwa wakimtimua
kila kona anayokaa tapeli huyo na kumtimua mbio kabla ya leo wananchi
hao kuamua kumkimbiza kutoka eneo la Hazina Ndogo hadi miyomboni na
kuanza kumpa kichapo hadi alipoamua kuonyesha viungo vyote kuwa si
mlemavu
Tapeli huyo mbali ya kujifanya ni
mlemavu wa viungo wakati mwingine huwa anajifanya ni mtu asiyeongea
(bubu) asiye na viungo kama mikono na miguu ila wakati mwingine
akijifanya ni hana mguu mmoja na kuwaomba watu fedha za matibabu .
Hata hivyo baada ya mmoja kati ya
wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya
mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa
mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao
huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo
mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa
akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)
Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo
ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja na
awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu
kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku
ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo kutokana na kichapo alichokipata
na kuumizwa vibaya usoni .
Hata hivyo inasemekana mzee huyo
amekuwa akiadhibuwa katika maeneo mbali mbali kutokana na mbinu yake
ya kufuru anayoifanya kuwa ni mlemavu wakati si mlemavu na kuwa ni
heri kuomba kama mtu mwenye matatizo ya kiuchumi kuliko kuwaigiza
walemavu na kuwa iwapo atarudia na kukutwa akifanya hivyo watamvunja
kweli mkono ili kuwa mlemavu walisema wananchi hao ambao hata hivyo
mtandao huu uliwaomba kufanya hivyo .
Aidha anadaiwa chanzo cha kichapo
cha leo kwa mzee huyo tapeli ni mmoja kati ya mpenzi wake ambae
alikuwa amemsusa na kuhamia kwa mpenzi mwingine kuueleza umma kuwa
huyo ni tapeli na yeye ni mpenzi wake ambae anamtambua kuwa na miguu
yote,mikono na si bubu kama anavyoigiza jambo lililopelekea wananchi
kufanya udadisi .
Kabla kufukuzwa na kuchezea kichapo
tapeli huyo alifukuzwa eneo ambalo alikuwa amekaa barabara eneo la
Santona na kutoka kuondoka haraka na mmoja kati ya vijana wanaofanya
kazi ya kusafisha na kushona viatu na kupuuza na ndipo mtiti ulipoanza.
Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi
wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa
wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka
kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada.
CHANZO: FRANCIS GODWIN WA MATUKIO DAIMA
CHANZO: FRANCIS GODWIN WA MATUKIO DAIMA
No comments:
Post a Comment