HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » FASTJET YANOGESHA SIKU YA MUZIKI DUNIANI, WASANII WAJIMWAGA KUTOA BONGE LA BURUDANI





Na Mwandishi Wetu
IKIWA juzi ilikuwa ni siku ya muziki duniani wasanii  mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya juzi walitoa burudani safi katika onesho la siku ya Muziki Duniani lililofanyika  katika viwanja vya Posta, Kijitonyama.
Tukio hilo lililodhaminiwa na kampuni ya ndege ya Fast Jet iliwahsirikisha wasanii Elias Barnaba, Godzila, Kala Jeremiah na wasanii wengine mbalimbali wa utamaduni.
Huku lengo lake ni kuwakutanisha wadau wa muziki pamoja na wasanii ikiwa pia na lengo la kuwa na mwelekeo mpya wa sanaa na muziki.
Pia katika kuongeza hamasa mfanyakazi wa kampuni ya Fast Jet Nyembo Mwiluka aliimba wimbo wake wa Njoo Turuke na Fast Jet.
Pia aliimba nyimbo zake nyingine mbalimbali huku akisindikizwa na madansa wake pamoja na wasanii wengine.
Tamasha hilo lilidhaminiwa na Fast jet, Alliance France, Goethe Institute na Pepsi ambapo hufanyika kila mwaka Juni 22.
Akizungumzia udhamini wake wa tukio hilo Meneja Biashara wa Fast Jet Jean Uku alisema kuwa kampuni hiyo mbali na kutoa huduma usafiri pia imeamua kusaidia masuala ya sanaa kwa kuwa inatambua nafasi ya sanaa katika kukuza ajira hususan kwa vijana.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: