Wakati
mitaa mingine ya katikati ya Jiji la Dar es salaam, ikiendelea kuwekwa
safi ikiwa ni maandalizi ya mapokezi ya Rais wa Marekani, Barack Obama,
Soko la Kariakoo
limesahaulika na kukithiri kwa Taka. Kamera yetu , leo ilivinjari maeneo ya Soko la Kariakoo majira ya jioni
na kukutana na kituko hiki, ambacho kinaleta kero kwa wananchi, abiria
wanaopandia daladala katika kituo hicho,
madereva wa wanaoegesha magari yao eneo hilo na wafanyabiashara wanaoshughulika katika eneo hilo, ambapo imeelezwa kuwa Taka hizo humwagwa eneo hilo na kuondolewa na magari ya Taka ambayo hupia mara moja kwa wiki, na muda mwingine hupita siku kadhaa zikiendelea kusota eneo hilo huku zikitoa harufu na kusababisha usumbufu mkubwa.

PICHA NA SOFIANI MAFOTO
No comments:
Post a Comment