*Maandalizi ya Obama yatikisa
*Siri yake nchini yatajwa
MAANDALIZI ya ziara ya Rais wa Marekani hapa nchini, Barack Obama yamezidi kushamiri na sasa Wamarekani ndio wanaoongoza karibu kila idara wakitumia vifaa vyao.
Eneo ambalo linaonekana kumilikiwa na Wamarekani kwa asilimia karibu zote ni lile la mawasiliano, ambapo inaelezwa kuwa maofisa wao ndio watakaoongoza kila kitu ikiwemo kufanya ukaguzi wa watu watakaoingia uwanjani hapo kesho kwa ajili ya kumlaki Obama.
Habari zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa kikao maalumu kimefanyika juzi, kikiwahusisha maafisa wa juu wa Marekani na Tanzania kwa ajili ya kutengeneza programu itakayofanikisha ziara ya rais huyo wakati atakapotua kesho na kuondoka Julai 2.
Kwa mujibu wa habari hizo ambazo pia zilithibitishwa na Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Moses Malaki zinaeleza kuwa maandalizi makubwa hadi kufikia jana yalikuwa tayari, ingawa kuna vifaa ambavyo Tanzania haikuwa navyo hivyo kuwaomba Wamarekani.

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Katika kikao hicho, inaelezwa kuwa maofisa wa Marekani ambao sasa wameteka karibu idara zote muhimu ambazo zitafanikisha usalama wa kiongozi wao, walihoji kuhusu huduma mbalimbali nchini na kutaka ipate orodha ya vitu vilivyopo na ambavyo havikuwepo.
Miongoni mwa vitu ambavyo vilikosekana au havikuwa katika hali nzuri ni pamoja na ngazi ya kushukia Obama kwenye ndege.
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi huyo wa uwanja wa ndege Malaki, alisema ngazi hiyo haikuwepo jambo ambalo liliilazimisha Marekani kuleta ya kwao.
MAGARI YA KUHIFADHIA MAFUTA
Maofisa hao pia walielezwa hakukuwepo na magari wanayoyataka wao kwa ajili ya kuhifadhia mafuta na hivyo kutakiwa kutumia ya Marekani.
MITAMBO YA MAWASILIANO
Upande wa mitambo ya mawasiliano, Malaki alisema kuwa imeongezwa ya kwao pamoja na iliyopo nchini.
Malaki alisema kwa kiwango kikubwa katika eneo hilo, Wamarekani ndio walikuwa wakilidhibiti kutokana na kuja na vifaa vyao vya kisasa

WAFANYAKAZI (JNIA) HAKUNA KUPUMZIKA
Malaki pia alisema kutokana na ziara hiyo ya Obama, hakutakuwa na mapumziko kwa wafanyakazi wa viwanja hivyo vya ndege mpaka kiongozi huyo atakapoondoka nchini.
Alisema kuwa watu pekee walioruhusiwa kutofika mahali pa kazi kuanzia siku ambayo Obama atawasili nchini hadi kuondoka, ni wanafunzi walio kwenye vitendo (field Attachment).
MTANZANIA Jumapili lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa wafanyakazi wa uwanja wa zamani (Terminal 1), ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini ambapo alilalamika kuwa amechoka na kazi kutokana na wageni wengi kuwasili uwanjani hapo katika kipindi hiki.

UKAGUZI KUFANYWA NA MAREKANI
Kuhusu suala la ukaguzi, Malaki alisema maofisa wa Marekani ndiyo watakaohusika katika zoezi hilo na kwamba watasimamia pamoja na kuwakagua watu wote watakaoingia kumlaki Rais Obama na familia yake.
“Ingawa tumeshirikiana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, lakini sehemu kubwa watafanya wao, wako ‘over safe’ kuna vitu ambavyo watafanya kuhusu usalama,” alisisitiza Malaki.

HALI YA BARABARANI
Barabara karibu zote katikati ya mji na kuelekea maeneo ya uwanja wa ndege, hali ya ulinzi ni ya hali ya juu.
Mapema jana asubuhi, maafisa wa polisi wa ngazi za juu walionekana kuwa kwenye kikundi katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere katika eneo la Tazara.
Pia askari wa usalama barabarani walionekana wakiwa katika vikundi vikundi na wengine mmoja mmoja kwa ajili ya kuhakikisha foleni haitokei pamoja na usalama.
MTANZANIA Jumapili lilishuhudia askari wengine wakiwa katika pikipiki pamoja na magari ya doria wakipita sehemu mbalimbali katikati ya mji na pembezoni.
Kwa upande wa vyombo vya ulinzi na usalama hususani Jeshi la Polisi, nalo habari zinaeleza kuwa hawatakuwa na mapumziko katika kipindi chote ambacho Obama atakuwepo nchini.
Wakati huo huo, habari ambazo gazeti hili imezipata zinaeleza kuwa miongoni mwa viongozi watakaokuwepo nchini kushuhudia ujio huo wa Obama ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya na mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Raila Odinga.
Hata hivyo juhudi za gazeti hili kumpata Odinga mwenyewe kuthibitisha juu ya taarifa hizo zilishindikana.
Odinga anatajwa kuwa na uhusiano wa karibu na Rais Obama, ambaye pia ana asili ya Kenya.

MTANZANIA
No comments:
Post a Comment