HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » BASI LA SUMMRY LAUA WATU 9 NA KUJERUHI 53


Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni na kuua watu tisana kujeruhi wengine hamsini na tatu.

Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa  jina la Ntungu

Alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko,  dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana 
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: