HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » HALMASHAURI NA MANISPAA ZIMEOMBWA KUTENGA VITUO VYAO RASMI VINAVYOTAMBULIKA KWA AJIRI YA BODABODA


Na John Banda,Dodoma.

HALMASHAURI za wilaya na Manispaa hapa nchini zimetakiwa kutenga vituo vya waendesha bodaboda kama ilivyo kwenye vituo vya teksi ili kuweza kuzuia uhalifu miongoni mwa madereva hao.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la Asasi inayojishughulisha na Rasilimali (Resources Network Foundation) (RNF) Ombeni Msuya kwenye hafla ya kuwasimika rasmi  na kuwaaga waratibu wa shirika hilo wa Mikoa na Wilaya hapa nchini.

Msuya alisema vijana waliojiajiri kwenye biashara ya bodaboda ni wengi na ndiyo nguvu kazi ya Taifa hivyo ni wajibu wa uongozi wa halmashauri za wilaya na Manispaa hapa nchini kuwatengea maeneo maalum ya kufanyia biashara zao ili kuzuia uhalifu.

Alisema ikiwa waendesha bodaboda watakuwa na vituo maalum vya kufanyia kazi zao wahalifu wanaotumia mgongo wa bodaboda watafahamika na hivyo vitendo vya uhalifu  vinavyofanywa na watu wanaojifanya ni madereva wa bodaboda vitakomeshwa.

“Hawa vijana waliojiajiri kwenye biashara ya bodaboda mimi huwa nawaita ni jeshi kubwa la ardhini kwa sababu wako kila kona ya Tanzania na ndiyo biashara ambayo hivi sasa vijana wengi wameweza kuajiriwa na kujiajiri hapa nchini hivyo Halmashauri na Manispaa zinatakiwa kuwatambua,” alisema Msuya.

 Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini


Aidha Mkurugenzi huyo amezishauri Halmashauri na Manispaa kuwapatia waendesha bodaboda hizo namba ili waweze kutambuliwa kirahisi pamoja na kuziweka alama pikipiki zao wanazofanyia kazi kwa lengo la kuwatambua zaidi hata pale inapotokea uhalifu na ajali badala ya kuwaacha wakifanya kazi zao kiholela.

Mbali na hilo Msuya aliwashauri waratibu hao kutumia fursa watakazokutana nazo katika maeneo yao katika kujipatia kipato chao cha kila siku kuliko kusubiri ajira kutoka serikalini.

Hafla hiyo iliwakutanisha vijana waliomaliza vyuo vikuu mbalimbali hapa mkoani Dodoma ambao ni wanachama wa RNF kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za shirika hilo sehemu mbalimbali ikiwemo mijini hadi vijijini.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: