YULE mchungaji wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania (EAGT) la Iwambi jijini hapa, Daniel Mwasumbi aliyekuwa akikabiliwa na skendo ya kubaka na kumpa mimba denti wa sekondari mwenye umri wa miaka 19, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12.
Mchungaji Daniel Mwasumbi akiwa chini ya ulinzi.
Akisoma hukumu hiyo mapema wiki hii, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Gilbert Ndeuruo alisema korti hiyo ilimtia hatiani mchungaji huyo kutokana na ushahidi uliotolewa na shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mwathirika wa tukio hilo.
Hakimu huyo alisema mtuhumiwa huyo alidaiwa kutenda makosa hayo kati ya mwezi Januari, mwaka 2008 hadi 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na sheria kifungu cha 130 (2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Binti aliyepewa mimba na Mchungaji akilia.
Kutokana na ushahidi huo, Hakimu Ndeuruo alidai kuwa mahakama yake ilimkuta mtuhumiwa na makosa mawili ya ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na mwathirika mwenyewe na mwalimu wa shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa shitaka lilidhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa upande wake, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana na mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti huyo wa miaka 19 huku mtuhumiwa akiwa na miaka 57.
Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa mchungaji huyo alimharibia binti huyo masomo na maisha ambapo vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbalimbali ikiwemo kanisani.
Endelea kusoma habari hii kwa kwa kubofya
Wananchi wakisubiri hukumu kutolewa.
Aliiomba mahakama hiyo kutaifisha vitu vya mchungaji huyo na kutoa amri ya matunzo ya mtoto.
Hakimu alimuuliza mtuhumiwa huyo kuhusu kupunguziwa adhabu ambapo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madai kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Mchungaji akitolewa kwenye chumba cha mahakama.
Kutokana na utetezi huo, Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ilihali katika kosa la pili alihukumiwa kifungo cha miaka mitano na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Sh. milioni 20 kwa fedha za Kitanzania kwa familia ya mwathirika huyo.
Hakimu huyo aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa.



No comments:
Post a Comment