HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MUDA WA KUOMBA MKOPO BODI WAONGEZWA


Veneranda Malima
Serikali imeongeza muda wa kupeleka maombi ya mkopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kwa wanafunzi watakaojiunga na mwaka wa masomo wa 2013/2014.


Hayo yalisemwa na Ofisa Habari Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Veneranda Malima alipokuwa akizungumza na NIPASHE, ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Alisema kutokana na baadhi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha sita kuchaguliwa kwenda kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), muda wa mkopo umeongezwa hadi Julai 31 mwaka huu.

“Tumetoa muda zaidi kwa ajili ya wale wanaokwenda kujiunga na JKT lakini ni fursa pia kwa wale ambao bado hawaja jaza fomu za kuomba mkopo,” alisema.

Alisema kuwa mwaka huu 2013/2014 wanakadiria kutoa mkopo kwa wanafunzi 35,000 kwa wale waliotuma maombi mapya na wale watakaothibitishwa kupewa tena.

CHANZO: NIPASHE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: