Dillish
Baada ya zile siku 91 zilizowaunganisha na kuwapa burudani waafrica kupitia ‘The Chase’ hatimaye jana (August 25) chujio la Big Brother kupitia kura za watazamaji limethibitisha nguvu ya wanawake katika shindano la mwaka huu baada ya Dillish Mathews kutoka Namibia kuwa ndiye mshindi wa $300,000 zilizowaniwa na washiriki 28 kutoka nchi 14 za Afrika ikiwemo Tanzania.
Ukweli ni kwamba shindano la mwaka huu lilikuwa ni zuri kwa namna yake kiasi cha kufanya kuwepo na ugumu wa kubashiri mshindi kutokana na jinsi ambavyo mchezo ulikuwa unaenda.
Mrembo Dillish amefanikiwa kuwapiga chini washiriki wenzake Cleo, Elikem pamoja na Wanaigeria Melvin na Bevelry walioingia tano bora. Dillish alipata kura 5, akifuatiwa na Cleo aliyepata kura 4, Elikem alikuwa nafasi ya 3 kwa kupata kura 3 na Melvin alipata kura 2 na Beverly aliambulia kura moja tu katika fainali ya jana.
Nafasi ya kwanza na ya pili mwaka huu zimekamatwa na wanawake, Dillish akiwa ndio mshindi katika nafasi ya kwanza na Cleo nafasi ya pili. Dillish amekuwa mwanamke wa pili kushinda Big Brother Africa baada ya mzambia Cherise aliyewahi kushinda taji hilo katika msimu wa kwanza wa BBA mwaka 2003.
Kura za jana zinaonyesha Afrika Mashariki yote Kenya, Uganda na Tanzania ziliungana na nchi za Angola na Namibia kumpa ushindi Dillish. Wanaigeria walimpa kura mshiriki wao mmoja Melvin huku Beverly akipewa kura moja na Ethiopia. Kura 3 za Elikem zilitoka kwao Ghana, Sierra Leone na ukweni Zimbabwe.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Hivi ndivyo kura zilivyopigwa:
Angola: Dillish
Botswana: Cleo
Ghana: Elikem
Kenya: Dillish
Ethiopia: Beverly
Malawi: Cleo
Namibia: Dillish
Nigeria: Melvin
South Africa: Cleo
Sierra Leone: Elikem
Tanzania: Dillish
Uganda: Dillish
Zambia: Cleo
Zimbabwe: Elikem
Rest of Africa: Melvin
Total: Dillish = 5, Cleo = 4, Elikem = 3, Melvin = 2, Beverly = 1.
No comments:
Post a Comment