HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MTAMBO MPYA WA KISASA WA KUBAINI DAWA ZA KULEVYA WAFUNGWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA (JNIA)



Rapiscan620dv (picha: www.rapiscansystems.com)

Ikiwa ni siku chache zimepita toka Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe afanye ziara ya kushtukiza katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es salaam (JNIA) kwa lengo la kujionea jinsi utendaji kazi unavyoendelea, Serikali imefunga mtambo mpya wa ukaguzi wa mizigo uwanjani hapo ili kusaidia mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya nchini.
Taarifa iliyoripotiwa na NIPASHE leo (August 26) inasema Serikali imefunga mtambo mpya wa kisasa utakazokuwa na uwezo wa kutambua dawa za kulevya zitakazoingizwa au kupitishwa kutoka ndani na nje ya nchi.

Uamuzi wa serikali kufunga mtambo huo umekuja kufuatia malalamiko kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) umegeuzwa njia ya kupitishia dawa hizo kwenda nchi za nje.

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini


Dk. Mwakyembe jana alifika katika uwanja huo kukagua mtambo huo wa Rapscan 600 series na kuelezwa na viongozi kuwa umetoka Uingereza na kufungwa kwenye uwanja huo kuanzia wiki iliyopita.
Dk. Mwakyembe akizungumza na NIPASHE katika uwanja huo baada ya kumaliza kukagua mtambo huo, alisema lengo la serikali kuongeza mtambo mwingine ili kukomesha kabisa tatizo la watu wasiokuwa waaminifu kupitishia dawa hizo katika uwanja huo na kuliletea aibu Taifa.
Alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa upande wake nayo imefunga mitambo yake kwa lengo la kukabiliana na dawa hizo na kwamba kutoka na ushirikiano uliopo katika ya vyombo vya usalama ni wazi kuwa itakuwa vigumu kwa mtu kuzipitisha JNIA.

Kwa upande wake Meneja Usalama wa JNIA, Clemence Jingu, alimweleza Dk. Mwakyembe kuwa mtambo huo umefungwa kitaalamu na kwamba hatua iliyobaki ni kufungwa kifaa kijulikanacho kama Soft narc scan.
Jingu alisema katika uwanja huo wameanzisha huduma ya kukagua mizigo ya abiria wanaoingia nchini kutoka nchi mbalimbali nyakati za usiku ambayo awali haikuwapo .


SOURCE: NIPASHE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: