Meneja wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amempinga aliekuwa meneja wa klabu ya Man Utd Sir Alex Ferguson kufuatia kitabu chake alichokizindua siku mbili zilizopita ambacho kinazungumzia maisha yake ya soka pamoja na changamoto alizokutana nazo wakati akifanya kazi hiyo.
Brendan Rodgers amempinga babu huyo alietangaza kustahafu ufundishaji wa soka mwezi May mwaka huu, kufuatia kumponda nahodha na kiungo wa klabu ya Liverpool Steven George Gerard kwa kumuweka katika kundi la wachezaji ambao hawapi kipaumbele cha kuonyesha viwango vya uhodari wa soka.
Rodgers pia ameupinga mwenendo wa Sir Alex Ferguson ambae pia amemponda kiungo mwingine wa klabu ya Liverpool Jordan Brian Henderson kwa kusema amekua akishindwa kurejea katika kiwango chake tangu alipojiunga na The Reds kutokana na majeraha yanayomikabili.
Rodgers amesema haamini kama kilichoandikwa katika kitabu cha mzee huyo mwenye umri wa miaka 71 kina mantiki kwa wadau wa soka duniani kote, kutokana na kila mmoja kumfajhamu vilivyo Steven Gerard kutokana na mchango wake mkubwa naoutoa akiwa na Liverpool pamoja na timu ya taifa ya Uingereza.
Amesema huenda yakaya maoni yake binafsia mbayo yanaonyesha ni vipi anavyomchukia nahodha na kiungo huyo wa The Reds ambaye kwa muda wote amekuwa akionekana imara anapokuwa uwanjani kwa kuhakikisha timu inafikia malengo yanayokusudiwa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kwa upande wa Jordan Brian Henderson,Brendan Rodgers amesema bado haamini kinachokusudiwa na Sir Alex Ferguson ambaye aliheshimiwa kutokana na mchango alioutoa katika medani ya soka nchini Uingereza kupitia Man utd.
Amesema kimtazamo kiwango cha Jordan Hernderson tangu alipojiunga na klabu ay Liverpool mwaka 2011 akitokea Sunderland, kimekuwa kikiendea vyema na hadhani kama kinashuka kama ilivyoelezwa na babu Ferguson.
No comments:
Post a Comment