HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MIILI YA MAGAIDI YAPATIKANA WESTGATE

 
Miili miwili iliyoungua vibaya aliyoopolewa katika eneo la kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya siku ya Alhamisi inawezekana kwa kiasi kikubwa ikawa ni ya magaidi walioshambulia kituo hicho, Mbunge mmoja wa Kenya ameiambia BBC.
 
Ndung'u Gethenji mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayochunguza shambulio hilo pia amesema mwili mwingine ambao umepatikana unawezekana kwa kiasi kikubwa ukawa ni wa mmoja wa wanajeshi.
 
Mamlaka ya Kenya kwa sasa inaendelea na uchunguzi wa kisayansi wa miili hiyo.
Karibu watu wapatao 67 walifariki dunia wakati magaidi wanaodhaniwa kuwa ni wa kundi la wanamgambo wa Al Shaabab waliposhambulia kituo hicho Septemba 21 mwaka huu.
 
 
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
Shambulio hilo lilisababisha eneo hilo kuzingirwa kwa siku nne ambapo pia sehemu kubwa ya kituo hicho cha biashara iliharibiwa.
Mamlaka ya Kenya imeyataja majina manne ya watuhumiwa wa shambulio hilo, japo hawajatoa ufafanuzi zaidi.
 
Bado haijajulikana kama magaidi waliofanya shambilizi hilo kama walitoroka au la na pia imekuwa ni vigumu kujua idadi ya magaidi waliohusika kwenye tukio hilo.
 
Awali maafisa wa serikali ya Kenya walisema inakadiriwa magaidi hao walikuwa kati ya 10 na 15 lakini picha za CCTV zilionyesha magaidi wapatao wanne tu ndo waliokuwepo kwenye tukio hilo.
 
SOURCE: ITV

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: