
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mtoto Joshua Isack (4) aliyepotea
nyumbani kwao akiwa anacheza na watoto wenzie kwa siku tatu akutwa akiwa
amefariki dunia ndani ya shimo la choo cha jirani na kuzua maswali ya
sintofahamu kwa wazazi na majirani.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Tukio hilo la kuonekana kwa mtoto huyo lilitokea jana majira ya saa Kumi jioni katika Mtaa wa Nyibuko Pambogo kata ya Iyela Jijini Mbeya baada ya juhudi za wazazi na majirani kushirikiana kumtafuta na kumpata akiwa amepoteza maisha ndabi ya shimo la choo.
Akizungumza kwa uchungu na masikitiko
makubwa baba mzazi wa marehemu Isack Daniel ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya
Maji Mbeya alisema Mtoto wake huyo wa kiume akiwa anacheza na wenzie jumatatu
ya Oktoba 28, Mwaka majira ya saa 12 jion lakini alitoweka katika mazingira ya
kutatanisha.
Alisema baada ya kuona giza linaingia na
mtoto hajarudi alianza kumtafuta katika kila eneo akishirikiana na baadhi ya
ndugu na majirani lakini hakufanikiwa kumwona kwa siku hiyo ambayo kesho yake
akiwa ni viongozi wa mtaa walienda kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Kati
Mbeya Mjini.
Alisema awali walivyopita siku moja
kabla waliona shimo hilo likiwa limefunikwa kwa mabanzi yaliyochakaa lakini
siku ya pili yake asubuhi walikuta kukiwa na mabanzi mapya kuashiria kuna
ukarabati umefanyika hali iliyowapa wasi wasi na kulazimika kulifunua shimo
hilo na kumkuta marehemu akiwa amepoteza maisha ndani ya shimo hilo.
Alisema aliyegundua kuwepo kwa mtoto
ndani ya shimo ni ndugu yakle alikuwa katika msako wa nyumba kwa nyumba na
ndipo alipompigia simu akiwa kazini nay eye kutoa taariofa polisi na kwenye
Serikali ya Mtaa ambapo walianza kufanya juhudi za kumtoa lakini walikwama hali
iliyowalazimu kuomba msaada kwa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji waliofanikiwa
kumtoa majira ya saa Kumi jioni.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa
wa Nyibuko Pambogo kata ya Iyela Mage Makwenda alisema akiwa ofisini kwake
alipokea taarifa za kupotea kwa mtoto katika mazingira ya kutatanisha lakini
wakiwa katika juhudi za kumtafuta ndipo walioteuliwa kufanya upelelezi na msako
mkali walipotoa taarifan za kuonekana kwa mtoto akiwa am,efariki dunia ndani ya
shimo la maji machafu.
Alimtaja mmiliki wa nyumba hiyo kuwa ni
Gesho Kibonde (43) mkazi wa Mtaa wa Nyibuko kata ya Iyela Jijini hapa ambaye
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano pamoja na mkewe.
Kwa upande wake majirani na wakazi wa
mtaa huo ambao hawakutaka majina yao kuandikwa walisema tukio hilo lina utata
mkubwa kwa sababu baada ya mtoto kuonekana ndani ya shimo baadhi yao
walifanikiwa kuchungulia na kumkuta marehemu akiwa amesimamishwa mithiri ya
kutumbukiwa na mtu.
Mashuhuda hao waliendelea kusema kama
mtotio angekuwa ametumbukia kwa bahati mbaya akiwa anacheza na wenzie
angeonekana kuumia baadhi ya viungo lakini haikuwa hivyo pamoja na kuonekana
kufa maji machafu ndani ya shimo hilo basi tumbo lake lingejaa lakini hali
aliyokutwa nayo marehemu ni tofauti.
Hata hivyo wengine wamelihusisha tukio
hilo na imani za kishirikina kwa madai kuwa aliyewaonesha kuwepo kwa mtoto
ndani ya shimo hilo ni babu kutoka Mwakaleli( mganga)ambaye alifuatwa na baadhi
ya watu ili kusudi awaoneshe mtoto na ndipobabu huyo alipowaambioa warudi
katika nyumba ya jirani watamkuta akiwa hai.
Walisema baada ya kurudi na kutafuta
katika eneo hilo waliokuta akiwa amekufa kitu ambacho waliamini ni kuchelewa
kufika na kuligundua eneo lakini wanrwahi huenda wangemkuta marehemu akiwa
mzima kabisa.
Aidha wakati zoezi la kumtoa marehemu
ndani ya shimo hilo kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi, Zimamoto na Uokoaji
pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mbeya(
Mbeya uwsa) vilio vilitawala eneo hilo kutoka kwa wanawake walioshindwa
kujizuia huku wengine wakipoteza fahamu na kulazimika kupewa msaada wa
kupepewa.
Na Mbeya yetu
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment