HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » AFARIKI GHAFLA NDANI YA GARI

 Picha  ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura  kutoka maktaba

Dar es Salaam.Mkazi mmoja wa Mapinga mkoani Pwani, Daniel Busiaye (58), amefariki dunia akiwa amekaa kwenye kiti cha gari eneo la Mbuyuni wilayani Kinondoni.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, tukio hilo lilitokea Novemba 10 mwaka huu.
Alisema mtu huyo ambaye wakati wa uhai wake alikuwa mfanyabiashara, alipanda daladala akitokea Mapinga kwenda katikati ya jiji.
Alisema gari lilipofika Mbuyuni njia panda ya Kunduchi, mtu huyo alianguka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekaa na kufariki dunia papo hapo.
Wambura alisema chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

MWANANCHI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: