Mvulana mdogo wa umri wa miaka (15) ana
uvimbe mkubwa Shingoni unaomsababishia kushidwa kupumua vizuri lakini
madaktari bingwa wanasema anaweza kutibiwa kwa kutumia Viagra.Jose
Serrano wa Ciudda d Juarez, Mexico alikuwa akiona ukuaji wa uvimbe
shingoni ukikuwa kila siku na kutishia maisha yake na ushauri wa
madaktari unasema oparesheni ya kawaida inaweza kuleta madhara katika
sehemu muhimu ya kiungo chake (shingo).
Taarifa zinasema kuwa ugonjwa huo
unajulikana kama (Lymphangioma) ni uvimbe ambao dawa yake ni Viagra
ambayo ni maarufu kwa kusaidia kuongeza nguvu za kiume lakini kwa upande
mwingine ni dawa ya uvimbe.Jose mwenyewe anasema kuwa ana matumaini
kuwa siku moja ataweza kuishi maisha ya kawaida kama vijana
wengine.
ENDELEA KUSOA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
"Kama madaktari wanaweza kunitibu mimi itakuwa ni siku ya
furaha, Napenda kuwa na afya na ningependa kuwa na uwezo wa kufanya kitu
chochote nikitaka," amesemaLakini wakati mwingine anapata huzuni kwa
sababu yeye ni tofauti na watoto wengine. Hadi sasa hatujapata fedha ya
kumtibu," amesema baba yake Jose Ramirez
CHANZO: DAILY MAIL




No comments:
Post a Comment