HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » BAADA YA KUZUNGUSHWA NA DAWASCO WANANCHI WA MWENGE NYUMA YA MAGHOROFA YA JWTZ WAAMUA KUJITOA MUHANGA NA KUSHIKA KINYESI KUZIBUA CHEMBA ZA MAJI TAKA, DAWASCO WAFIKA KWA KUCHELEWA.

Mmoja wa wakazi wa mtaa huo aliyeamua kujitoa na kushika kinyesi ili apate  kuzibua chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji bila kusimama kwa siku Sita
Hali hii ilikuwa mbaya jambo ambalo wananchi waliamua kujitolea na kufanya wawezalo ili kuzibua
Hali ni Tete eneo hili ambapo sasa moja ya Chemba inazidi mwaga maji na hapa kila mtu anatoa wazo lake nini kifanyike ili kuweza kuzibua eneo hilo ambalo  maji yake yalikuwa hayapungui kumwagika bali kuongezeka..na mwisho wote waliona bora washike kinyesi kuliko kuendelea kuteseka.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Ilikuwa ni baada ya kuhangaika sana wakazi wa eneo hili kwa kutumia nyenzo yao Duni ya nondo maalumu ya kuzibulia chemba waliyoinunulia wenyewe,hatimaye  walifanikiwa kuzibua chemba moja na kuhamia chemba ya pili .
Baada ya Chemba ya Juu kuzibuka , kasheshe ikahamia katika chemba ya pili ambapo sasa maji yote yalihamia hapo.
 Masikini mtazame Mama huyu alivyo Ruka juu na mtoto akiwa amemshika kihatari namna hii, hii ni adha ya haya maji taka.
 Wakazi wa eneo hili wakiwa wanakomaa kwa nguvu zote kuanza kuzibua chemba ya pili.
Zoezi sasa linaendelea na hapa walikuwa wanaendelea kuzibua chemba ya 3  ambapo sasa  walifika kikomo baada ya kuonekana chemba hiyo ilikuwa  imejaa matakataka ya kutosha pamoja na Mchanga . Na ndipo walipo pata taarifa kuwa DAWASCO wanakuja.
Wakiwa wamefika  kabisa na kujionea adha ya kukanyaga maji Taka huo nyuma ni mtambo maalum wa kuzibua Chemba 
Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wamefika katika eneo la tatizo na kuanza kuzibua  chemba za maji taka ili kuwasaidia wakazi hao wasipatwe  na magonjwa , Kero ya maji mtaani na harufu mbaya
 Wakiwa wanahakikisha kabisa kwamba tatizo limekwisha eneo hilo.
Moja ya Chemba ambayo wakazi wa Mwenge walikuwa wamehangaika nayo sana mpaka kufanikiwa  kutoa maji taka hayo  yaende ikiwa inaangaliwa na wafanyakazi wa DAWASCO
 Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wanaendelea kutoa takataka katika chemba sugu ili kuruhusu maji yapite
 Hii ni Baada ya Chemba Kuzibuliwa na wananchi wakishirikiana na DAWASCO Ambao walichelewa kufika eneo la tukio
 Maji yakionekana yanaendelea kukauka baada ya Chemba hizo kuzibuliwa
Hizi ni Takataka zilizo bakia baada ya kuzibua Chemba hizo ... 

Wananchi mtaa wa mwenge  waandamana na kufanya usafi kufuatiwa na kero kubwa ilyokuwa sugu na hatari katika afya zao, kero hiyo ikiwa ni kuziba na kufumuka  kwa chemba zinazo pitisha maji machafu maarufu kama  (majitaka )


Ikiwa nizaidi ya wiki mbili wakazi na watumiaji wa njia ya mwenge katika mtaa huo uliogeuzwa jina na kupewa jina mahususi na mazingira ya mtaa ambalo ni mtaa wa( kinyesi street) wamekumbwa na kero ya kufumuka kwa chemba za maji taka na kuwa na harufu mbaya  hivyo wananchi wamehofia afya zao nakuanza kuzibua Chemba za maji hayo huku kila baada ya mwezi huletewa  Bili na kuweza kuzilipia bila ya wasiwasi .Lakini kibao kimegeuziwa kwa wananchi kuwa ndio wamiliki wa shirika la maji safi na taka (DAWASCO) leo hii waamua kuondoa adha hiyo iliyo dumu kwa muda mrefu bila ya ufumbuzi kwa kushika Kinyesi na maji machafu kutoka sehemu mbalimbali.


Hata hivyo wakazi walilalamika kuhusu  utendaji kazi wa dawasco kuwa ni mbovu kwa kuwa wame watafuta zaidi ya
mara kadhaa  bila mafanikio


Aidha wananchi walionekana kuwa na moyo mmoja wa ushirikiano kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka katika chemba hizo nakufanikisha kuzibua chemba zote katika mazingira magumu yanayo weza kusababisha maradhi
mbalimbali kwa jamii husika wameongeza kuwa wana iomba mamlaka ya maji (DAWASCO) hususani kitengo cha majitaka kuweza kupita kila baada ya wiki moja ili kuweka mazingira mazuri/safi. PICHA NA DAR ES SALAAM YETU

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: