BUNGE la nchini Kenya leo Novemba 13 limepitisha muswada wa ugavi wa mali kati ya wanandoa baada ya kutalikiana.
Muswada huo unaeleza kwamba mwanamume au mwanamke atapata sehemu ya
mali aliyochuma wakati wa ndoa iwapo wataamua wanandoa watamua
kuachana.
Katiba ya sasa inaeleza wazi kuhusu haki sawa kati ya wanandoa
kabla,wakati na hata baada ya kuvunjika ndoa. inaeleza kwamba mali
inayomilikiwa wakati wa ndoa itagawanywa nusu kwa nusu baina ya mume na
mke iwapo wataachana.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wabunge wanawake nchini humo wanataka muongozo usalie kama
ulivyo,Idadi kubwa ya wabunge wanaume walipiga kura kwa uwingi wa kura
87 dhidi ya wabunge wanawake 28 kuibadili sheria hiyo.
Sehemu kubwa ya wabunge wanawake waliwashutumu wenzao wanaume kwa kupitisha mswada huo ambao wameutaja kwenda kinyume na katiba.




No comments:
Post a Comment