Pamoja na kuwa
kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana
kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume.
Kwa kiasi kikubwa
katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao
hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi kukana na
shamra shamra anazokuwa nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa
na Harusi.
Hata hivyo, kwa
wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya
sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni
kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)
1. Vigezo
vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake wengi
hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika
kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe
mume wake.Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo
huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo.
Vigezo
hivyo huwa hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo, kuna wale ambao
hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua,
mtanashati, sauti nzuri n.k.
Inaweza kuwa
kama mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao
anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile
ambavyo yeye anataka mumewe awe.
2. Kutaka
mwanaume tajiri
Kuna wanawake ambao
tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule
ambaye hana pesa nyingi.
Yupo
tayari kuolewa ila si kwa mwanaume mwenye uwezo wa kawaida, hata ikitokea
mwanaume ana uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona huyo
mwanaume hamfai hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi maisha ya
kifahari.
Hivyo
hukazana kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa na
uwezo mkubwa, bila kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.
3. Kutompata
Mwanaume Ampendae
Hili ni
kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani na haifai bali
tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini anakupenda
pia.
Wengi
katika kundi hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni kupendana tu
na mengine hufuata kwenye sababu ya upendo. Kunawanawake vigezo vya
mwanamme awe vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa.
Yeye
kikubwa anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na
matumaini kuwa huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu
mwanamke anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe
basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo atakapokuwa
tayari kuolewa.
4. Kuchagua
mno Wanaume wa Kumuoa (SO SELECTIVE)
Kuna wale
wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga; wasioridhika wala
kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa aina ipi wanataka.
Akija wa
mwenye uwezo atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo atatoa sababu
tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta maendeleo.
Akija wa
kabila hii, atasema hapana hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa
ufupi ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa.
Hatimaye
inaweza tokea muda wa kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini
ikiwa hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika soko.
5. Kujiona
ni mzuri sana
Kuna wanawake ambao
ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni
mzuri kiasi kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na
hata wote kumtamani.
Hata
hivyo hapo hapo kuna wale ambao huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamowake hujiona
ni mzuri mno hakuna mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi
hili hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu
anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana.
Kitendo
hiki hukuza nyodo za hali ya juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba
wanapojitokeza wanaume kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau
na kiburi.
6. Kujiona
ana Umri mdogo
Binti
yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa.
Wanawake wametofautiana
mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa hutamani
sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi.
Katika
kundi hili umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka
25 na bado akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona
ni mkubwa na anafaa kuolewa.
Hii pia ni
kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha
katika ndoa.
Anapokuwa
na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni
kikwazo kwake kuingia katika ndoa.
7. Maradhi
hasa UKIMWI
Hili kama
lilivyo kwa wanaume - Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa
maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano
na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua
kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na
mtoto.
Wengi
sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa,
hasa tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya
hudhoofika zaidi
8. Kutaka
maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana
na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi
zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya
tamthilia yawe na kwao pia.
Hilo
linafanya vigezo ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume
kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia.
Wengi
hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya
maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi kiigwe na
kipi kiachwe kama kilivyo.
9. Kuona
taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo
huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:
·
Usomi: Aina ya usomi ambao
hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na
mengine mengi.
·
Kushuhudia ndoa mbovu: Hii
inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe (pengine mama aliteswa
sana), na hata ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake
anayoijua mwanamke huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa.
·
Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya
lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume
kwake anaona kama ni utumwa.
10.Kutokuwa
kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake wale
wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata
hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi.
Wengi wa aina hii
ya wanawake huwa ni waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa
wale ambao wamewahi hata jaribu baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero,
unyanyasaji na uchafu.
Hivyo wazo la kuwa
akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa
hamu ya kutaka kuolewa.
No comments:
Post a Comment