Baada ya kuwakaribisha Dar, rapper kutoka jiji la miamba Kala
Jeremiah amepanga kuachia wimbo mpya alioupa jila la ‘Wale Wale’
sambamba na video yake November 20 mwaka huu.
Katika wimbo huo ambao amemshirikisha Nay Lee, Kala Jeremiah amesema utahusu maisha ya kila siku ya watanzania.
kupitia Instagram, Kala Jeremiah ameandika:
"TAREHE 20 MWEZI HUU WA 11 MWAKA HUU WA 2013 JUMATANO YA WIKI IJAYO
WIMBO WANGU MPYA UNAOKWENDA KWA JINA LA WALE WALE NILIOMSHIRIKISHA NAY
LEE UNATOKA RASMI AUDIO NA VIDEO KWA PAMOJA ASANTENI SANA."




No comments:
Post a Comment