Dadaab, moja ya kambi kubwa wanakoishi wakimbizi wa Somalia.
Zaidi
ya wakimbizi 500,000 wasomali wanaoishi nchini Kenya, wanatarajiwa
kurejeshwa makwao Somalia, baada ya shirika la kuwahudumia wakimbizi hao
la UN kutia saini mkataba na Kenya pamoja na Somalia kuhusu kuwarejesha
nyumbani wakimbizi hao.
Wasomali hao watarejeshwa kwa hiari nchini Mwao katika kipindi cha miaka mitatu inayokuja.
Wasomali wamekuwa wakitafuta hifadhi nchini Kenya kutokana na vita na umasikini nchini Somalia.
Kambi mbili ambako wakimbizi hao wanaishi, Dadaab na Kakuma
zinafanana na miji mikubwa kwa ajili ya idadi kubwa ya wakimbizi hao.
Baadhi ya wakimbizi pia wanaishi katika mtaa wa Eastleigh mjini
Nairobi ambao unajulikana kama Somalia ndogo kutokana na idadi kubwa ya
wasomali wanaoishi mtaani humo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wakimbizi wengi kutoka Somalia walitoroka kutokana na vita, baada ya serikali kuporomoka mwaka 1991.
Wengi wao walizaliwa kambini na hawajawai kamwe kwenda Somalia.
Serikali za Kenya na Somalia pamoja na UN zimeanzisha rasmi mpango
wa kuanza maisha mapya nchini Somalia na kushiriki katika mpango wa
kujenga upya nchi yao.
Naibu waziri mkuu wa Somalia Fowsia Yusuf Adam, alisema Serikali inajiandaa kuwapokea raia wake waliokuwa wanaishi ukimbizini.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa makubaliano ya kuwarejesha wakimbizi
Somalia ni wito kwa jamii ya kimataifa kujitolea kutafuta suluhu la
kudumu kwa mzozo ambao umeendelea kwa miaka mingi bila kikomo.
Hata hivyo changamoto ni kuwa mkataba huo unawataka wakimbizi
kurejea kwa hiari ingawa wengi wanaona Somalia bado ni mahala pasipo
salama na hivyo itakuwa vigumu kwao kurejea.
BBC SWAHILI




No comments:
Post a Comment